Matokeo EDK Darasa la saba 2021 haya hapa, Ufaulu wapanda
Ufaulu EDK
Darasa la Saba waongezeka
Na Bint Ally Ahmed
KIWANGO cha ufaulu
wa Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Dini ya Kiislamu nchini (EDK) kwa mwaka 2021,
kimeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana 2020.
Kwa mujibu wa
taarifa ya Katibu wa Islamic Education Panel, Mwalimu Shafii Hussein
iliyotolewa Septemba 9, 2021, kiwango cha ufaulu EDK kimeongezeka
kutoka wastani wa asilimia 46.27 mwaka 2020 hadi kufikia
wastani wa asilimia 49.78 kwa mwaka 2021.
“Kiwango cha ufaulu
katika mtihani wa Elimu ya Dini ya Kiislamu kwa wahitimu wa Darasa la Saba
uliofanywa Agosti 11, 2021 kimeongezeka kutoka wastani wa
asilimia 46.27 mwaka 2020 hadi wastani wa asilimia
49.78 mwaka 2021.“ Ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo
imesema, jumla ya watahiniwa 126,088 waliosajiliwa walifanya mtihani huo wa
kuhitimu wa Elimu ya Dini ya Kiislamu kwa Halmashauri 164 mwaka 2021 sawa na
asilimia 12.33
Mikoa 30 imefanya
mitihani hiyo, ambapo wameongezeka watahiniwa 5,893 sawa na asilimia 4.90
kutoka watahiniwa 120,195 mwaka 2020 hadi watahiniwa 126,088 mwaka 2021.
Taarifa hiyo imetaja
Shule bora 18 zilizopata wastani wa juu kabisa unaolingana kwamba ni Al Aqabah
(Mororgoro), Al Jazira (Ruvuma), Al Hudhaifa (Kagera), Answaar (Dar es
Salaam), Green Valley (Arusha) na Shule ya Msingi Hedaru iliyoko Same
Kilimanjaro.
Nyingine ni shule ya
msingi Ilala iliyoko jijini Dar es salaam, Islamiya (Nyamagana Mwanza),
Kilimanjaro (Arusha), Kyenge Islamic Primary School (Bukoba Vijijini), Lowjoma
(Ilemela Mwanza), Muzdalifa (Korogwe), na Muzdalifa (Newala Mtwara).
Shule nyingine
zilizofanya vizuri ni, Muzdalifa (Tanga Mjini), Sengerema (Sengerema Mwanza),
Sirajul Munir (Kiwangwa iliyoko Chalinze Pwani) na Shule ya msingi Temeke
Islamic, iliyopo Temeke Jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo
imefafanua kuwa, Halmashauri kumi bora ni zile zenye wastani wa juu Zaidi,
ikiongozwa na Mbinga Mjini, Korogwe Mjini, Arusha Vijijini, Dododma Mjini,
Geita Mjini, Ukerewe, Namtumbo, Bukoba Vijijini, Sengerema na Mbeya Mjini.
Taarifa imeongeza
kuwa mikoa imepangwa kuanzia mkoa wenye wastani wa juu hadi mkoa
wenye wastani chini kabisa ambapo Mkoa wa Kusini Pemba una wastani wa 79.16,
Kaskazini Pemba 76.52, Njombe wastani 61.78 Songwe wastani 60. 54, Kusini
Unguja wastani wa 60.54, Mjini Magharibi (Unguja) wastani wa 60.50,
Kagera 58.70, Kaskazini Unguja 55.92, Arusha 55.30, Mwanza 54.80 na
Mtwara wastani 53.00.
Dar es Salaam ina
wastani wa 51.36, Pwani 51.24, Lindi 50.82, Kilimanjaro 50.26, Morogoro 50.00,
Rukwa 49.96, Dodoma 48.46, Tanga 47.72 na Geita 47.66.
Mikoa iliyofuatia ni
Kigoma ikiwa na wastani wa 47.54, Manyara 47.40, Tabora 47.30, Katavi wastani
47.24, Iringa wastani 47.06, Shinyanga wastani 47.00, Ruvuma 46.24, Mbeya
44.36, Singida 42.32 na Mara wastani wa 40. 78.
Matokeo kwa kila
shule yanapatikana katika tovuti ya Islamic Education Panel
Hakuna maoni
Chapisha Maoni