Andalusia waja na kongamano la ndoa, Mufti Mgeni rasmi
Mwandishi wetu
Mufti na Sheikh Mkuu waTanzania
Sheikh Abubakar Zubeir anatarajiwa kuongoza jopo la masheikh wa Jiji la Dar es
salaam na Viunga vyake katika kongamano maalum la wanandoa lililoandaliwa na
kituo cha mafunzo cha ANDALUSIA linalotarajiwa kufanyika Septemba 26, 2021
katika ukumbi wa DYCCC uliopo Chang’ombe Jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa mwanakamati ya
maandalizi ya kongamano hilo, Akhy Said Salim Khamis, amesema Mufti atafungua
kongamano hilo na kuzindua kozi rasmi ya mafunzo ya ndoa(fiqhi ya ndoa) inayotarajiwa
kufanyika kila maeneo inshaa allaah.
Aidha amewataja walimu wanaotarajiwa
kutoa mada kuwa ni pamoja na Sheikh Muhammad Iddi (Abuu Iddi) ambaye ataeleza
MAKOSA YANAYOFANYIKA KABLA NA BAADA YA NDOA, lakini pia atakuwepo Sheikh
Muharami Mziwanda ambaye atazungumza mada NINI MAANA YA NDOA?
Wengine ni Sheikh Othman Khamis, Imam
wa msikiti wa Mtoro ataezungumzia mada ya VIPI TUTAWEZA KUZITUNZA NDOA ZETU
pamoja Sheikh Abdulrahman Muhina maarufu baba Kiruwasha(babie sheghele)ambae
atawasilisha mada: UTAMU KATIKA MAISHA YA NDOA MAMBO NI HUKU NA HUKU ambao
wamejianda vilivyo kufikisha daa’wah kwa wataohudhuria.
Amewashauri waislam na wasio waislam
kuchachangamkia fursa kusiriki kongamano hilo na kujiunga na mafunzo ya
kufahamu ndoa kiujumla,kwani itasaidia kuimarisha ndoa ambazo zinalegalega
lakini pia kukinga ndoa za wapendanao wanaotaraji kuingia ndoani.
Said Salim Khamis albakry ambaye pia
ni Mudir(Mwalim Mkuu) wa Madrasat IHSAANIYYAH (tandale) amesema: mafunzo hayo
yatatolewa kwa kushirikiana na Baraza kuu la waislamu Bakwata na wameweka
kiingilio cha shilingi elfu kumi na tano 15000/kwa ajili ya kuchangia gharama
za uandaaji pamoja na chakula kwa washiriki wote pamoja na vinywaji.
Aidha akizungumzia kwanini wamekuja
na kongamano hilo,Akhy Said salim alisema: "kwa sasa kumekuwa na tatizo
kubwa la ndoa nyingi kuvunjika jambo ambalo ni kinyume na maisha walioishi
wazazi wetu".
Alisema wazee wa zamani walifanikiwa
kuishi pamoja hadi uzeeni,waliweza kuzikana lakini vijana wa sasa wameshindwa
kufikia mafanikio hayo huku chanzo kikubwa kikitajwa kuwa ni ukosefu wa elimu
ya ndoa.
Ameongeza kusema ndoa nyingi zimekuwa
ni kaa la moto,wengine wamekuwa wakiishi kwa mazoea au pengine kuogopa kuwatesa
watoto jambo ambalo wamebaki hawana amani ya ndoa bali wanaishi kama wapo
katika gereza.
“Changamoto iliyopo sasa katika jamii
ni kukosa mafunzo ya ndoa,ikiwa leo mtu akitaka kufuga lazima akasomee kozi ya
ufugaji,mtu akitaka kuendesha gari lazima akasomee kozi ya udereva vile vile
mtu akitaka kuswali lazima asome Fiqih za swala, vipi kuhusu elimu ya ndoa?
ndoa ambayo ni maisha ya kudumu kwa watu.
Kubwa ambalo limeondoka kwetu ni
kukosa mafunzo thabiti ya ndoa,ukiangalia hata katika mitandao ya kijamii,meza
za masheikh,hata kwenye maofisi ya serikali kuna mmomonyoko wa maadiili,sababu
kubwa ni kukosa elimu sahihi ya mafunzo ya ndoa.
Sisi ANDALUSIA kwa kushirikiana na
Baraza la waislam Tanzania (Bakwata) chini ya usimamizi wa samaha mufti sheikh
ABUUBAKAR ZUBEIR tumeona ni vizuri kuandaa semina ili kusaidia kuponya ndoa
nyingi lakini pia kuwa kinga kwa wanandoa wapya na wanaotarajia kuingia katika
ndoa,” alisema Mwenyekiti wa kitengo cha wanawake Khadija Ali Alwi.
Kwa upande wake Imam wa msikiti wa
Mtoro, Sheikh Othman Khamis amekiri kuwa atakuwepo siku ya tukio na kuwaomba waislamu
kujitokeza kwa wingi kupata faida ya semina hiyo.
Amesema semina kama hizo ni muhimu
kwa afya ya ndoa, kwani jambo la ndoa ni kubwa na linahitaji kujifunza kama
zilivyo taaluma zingine.
Naye Khadija Abubakar Amri, Mjumbe wa
kamati ya maandalizi ya kongamno hilo amesema maandalizi yote yako vizuri
wanawaomba wananchi kujitokeza ili kupata mafunzo hayo.
Faiza Bathigili nae pia amesema kwa
sasa Tanzania ndoa nyingi ziko matatizoni na kwamba kuwa uhitaji mkubwa wa
jamii kupata elimu zitakazowasaidia kuponya ndoa zao.
Amesema kuna baadhi ya nchi ikiwamo
Malysia na Zanzibar na indonesia wamefanikiwa kupunguza tatizo la talaka kwa
jamii kwa sababu ya uwepo wa semina za na kozi za ndoa ndoa kwa kila mara.
Kongamano la wanandoa linatarajiwa
kufanyika Jumapili ya Septembea 26, 2021 katika ukumbi wa DYCC uliopo
Chang’ombe Jijini Dar es salaam, kiingilio katika semina hiyo ni shilingi
15,000/= kwa mtu mmoja na kwa shilingi 25,000/= kwa watu wawili.
Pia Mwenye kiti wa Andalusia KHADIJA
ALI ALWY anawakaribisha sana katika kongamano hili na kozi zitapoanza katika
vituo husika,na tickets zinapatikana andalusia upanga na k/koo.
Kwa mawasiliano na kwa anaetaka
ticket tafadhali wasiliana na ANDALUSIA kwa namba za simu:
0784302232/0716561347
Hakuna maoni
Chapisha Maoni