Chama cha soka la wanawake Tanzania (TWFA) kimevitaka vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa kuacha kuigombanisha na Raisi Mama Samia Suluhu Hassan kufuatia kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kuwa wachezaji wa timu hiyo wana muonekano kama wanaume.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wa timu hiyo, Janeth Christopher alisema kauli hiyo imetafsiliwa kisiasa na kusababisha mjadala mzito ambao umekua hauna tija kwa taifa huku akiviomba vyombo vya habari kujadili kauli ya rais Samia kwa  mtazamo chanya, nakuacha kuwagombanisha wachezaji hao na Rais Samia Suluhu.

Alisema kauli hiyo ilikua na nia ya kuwapa chachu wachezaji hao ili wafanye vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na kwamba wataendelea kufanya mazoezi ya nguvu ili kuendelea kua imara kiafya nakwamba suala la muonekano wao kama wanaume halitawafanya washindwe kushiriki vyema kwenye michuano.

Awali Mchezaji  Ester Mabanza alisema Rais Samia Suluhu Hassani amekua mfadhili wao mkubwa tangu akiwa makamu wa rais kipindi cha serikali ya awamu ya tano ya raisi Dkt. Jonh Magufuli hivyo wataendelea kushirkiana nae katika kukuza soka la wanawake nchini.

"Mama Samia ni mama, mlezi na ni Mkuu wa Nchi pia, kwahiyo sisi kutuasa ni jambo la msingi sana, tumepokea ushauri wake na sisi tutaendelea kushirikiana nae " alisisitiza Ester Mabanza.