Zinazobamba

Msingoje ajira, fanyeni ujasiliamali

 



Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali za vitega uchumi zilizoko nchini ili kukabiliana na changamoto za maisha zinazolikabili taifa hususan katika kundi hilo


Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mtendaji wa Mummys  Confectionery Company ltd, Bi Munira Ndossy katika wiki ya maonyesho ya Biashara na Viwanda ya Afrika Mashariki.
Alisema Vijana hususani wa kike kuchangamkia fursa mbalimbali zilizo patikana katika maeneo yao badala ya kukaa kungojea kuajiliwa.

"Nitoe rai kwa vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika maeneo yao ili kuweza  kufikia ndoto zao badala ya kukaa kungojea nafasi za ajira ambazo ni chache" Alisema Munura.

Alisema kitu cha msingi kwa vijana ni kuwa na wazo na jinsi ya kulisimamia wazo hilo kuweza kutekelezeka ukishawezaa kusimamia wazo lako na kuangalia fursa zilizopo ni rahisi kufanikiwa

Bi Munira aliongeza kuwa pamoja na dhamira nzuri na ya dhati iliyonayo serikali kuhakikisha inaboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara bado kumekuwepo na changamoto hasa kwa wafanyabiashara wadogo  na wakati.

Aidha aliongeza kuwa kampuni yake imekuwa ikijikita zaidi katika uzalishaji na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya mipaka ya tanzania kama India.

Akizungumzia mazingira ya ufanyaji wa biashara mkurugenzi huyo ameishukuru  TCCIA kwa jinsi ambavyo wamekuwa msaada kwao na wafanyabiashara wadogo kuweza kuwapa mwongozo wa kuwawezesha kufanya biashara zao.
 

Hakuna maoni