KITUO CHA TAARIFA NA MAARIFA SARANGA CHAWAFUNDA WAJASIRIAMALI SOKO LA TEMBONI, IKIWA NI MREJESHO WA MAFUNZO WALIYOPEWA NA TGNP.
Makamu Mwenyekiti wa kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Saranga Maria Mwigune akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wafanyabiashara wa soko la Kimara Temboni. |
Wafanyabiashara
wa sokoni wametakiwa kuendele kutumia njia za asili za kusindika mboga na
matunda ili kuondokana na hasara zisizo za lazima kwa kutupa bidha hizo zinaponyauka
au kuoza.
Hayo
yameelezwa jana Julai 23 na Makamu Mwenyekiti wa kituo cha Taarifa na Maarifa
kata ya Saranga Maria Mwigune, wakati kituo hicho kikitoa elimu kwa
wajasiriamali wa Soko dogo la Kimara Temboni juu ya usindikaji wa mboga na
matunda.
Aidha Makamu
Mwenyekiti huyo amesema kuwa wao kama kituo wameamua kuwafundisha wajasiriamali
hao baada ya wao kupewa elimu hiyo na shirika lisilo la kiserikali ambalo ni
TGNP, Na hii ikiwa ni sehemu ya mrejesho wao wa mafunzo waliyopewa julai 15
mwaka huu.
Ameongeza
kuwa mbinu hizo walizowapa za kusindika zitawasaidia wafanyabiashara hao kwani
mboga na matunda uweza kukaa kwa muda mrefu Zaidi bila kuharibika na wataweza
kuepukana na hasara za mara kwa mara za kutupa mboga, Na kuongeza kuwa njia
hiyo inatumiwa pia na maduka makubwa (supermarket) ya ndani na nje ya nchi.
Amesisitiza
kuwa licha kutoa elimu ya ujasiriamali lakini pia wametoa elimu ya ukatili wa
kijinsia kwa kwani maeneo ya sokoni vitendo hivi vinakuwa vingi hasa rushwa za
ngono na ukatili wa kiuchumi, Na kuwafundisha endapo tukio hilo litatokea nini
wafanye au wakatoe ripoti wapi.
Na mwisho
ameongeza kuwa amefurahishwa na muitikio wa washiriki kwani wamepata watu Zaidi
ya 100 na hasa wababa wamejitokeza kwa wingi sana, Hii inaleta picha nzuri kwa
kuona vitendo hivi vya ukatili tunakwenda kuvitokomeza na kuvisambaratisha
kabisa.
Mwenyekiti wa soko la Temboni Bi. Erineka Lyimo akiongea na washiriki wa semina ya kuwajengea uwezo wajasiriamali wa soko hilo. |
Kwa upende
wake Mwenyekiti wa soko hilo la Temboni Bi. Erineka Lyimo amesema kuwa elimu
hiyo waliyopata itawasaidia watu wake kwa Nyanja zote kwani mambo yakutupa tena
mboga wala matunda hayatakuwepo, lakini pia vitendo vya ukatili vitapungua
kuanzia hapo sokoni mpaka majumbani kwani hata wababa wamejua pa kupeleka
malalamiko yao endapo watanyanyaswa na wenza wao.
Ameendelea
kusema kuwa amefurahishwa pia na somo la bidhaa za urembo wa asili(culture)
kama hereni na Vidani kwani wanawake wengi watapunguza muda ya kupiga umbea na
badala yake watafanya kazi ya kutengeneza hivyo vitu ili kujiongezea kipato
chao.
Na mwisho ametoa wito kwa wanaume wasione aibu kuwasilisha malalamiko yao endapo watafanyiwa ukatili wa aina yoyote na kutoa ahadi ya kuwa wao kama wajasiriamali wadogo watazidi kuisambaza elimu hiyo mbali Zaidi ili jamii iweze kunufaika na elimu hiyo.
Mwanaharakati wa Masuala ya kijinsia Hance Obote akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko dogo la Kimara Temboni mapema jana mkoani Dar es salaam. |
Washiriki wa semina wakifuatilia mafunzo kwa umakini. |
Semina ikiendelea. |
Mjasiriamali Hussein Said akiwafundisha wafanyabiashara wa soko la Temboni namna ya kutengeneza bidhaa za kitamaduni (culture) mapema jana mkoani Dar es salaam. |
Washiriki wa semina wakiwa katika picha ya pamoja mapema jana mkoani Dar es salaam. |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni