Viongozi wa Dini waiomba Serikali kuharakisha usikilizaji kesi za viongozi, wakemea matusi kwa viongozi wastaafu
Hussein
Ndubikile, Dar es Salaam
Ombi hilo limetolewa
jijini Dar es Salaam na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeiry
baada ya Kikao kilichowakutanisha viongozi hao kumaliza kikao kilichojadili
masuala mbalimbali ikiwemo kujenga undugu kati ya waamini wa dini zote,
mustakabali wa taifa na kuhamasisha kudumisha amani, umoja na mshikamano.
Amesema kuwa
anaiomba mahakama na MKurugenzi wa Mashtaka na Serikali kwa ujumla kuharakisha
usikilizaji wa kesi wa viongozi wa dini kwani wameshikiliwa kwa muda mrefu bila
kujua hatma zao.
" Tunaiomba
mahakama, DPP na Serikali itatue kesi zikilizwe kwa haraka watakaokutwa na
makosa wachukuliwe hatua za kisheria," amesema Mufti Bin Zubeiry.
Amebainisha kuwa
viongozi wa dini wanaoshikiliwa na vyombo vya sheria watendewe haki kwa
kusikilizwa kesi zao kwani kuwaweka ndani muda mrefu ni kuwanyima haki zao za
msingi.
Kwa upande wake
Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki
na Pwani, Dkt. Alex Malasusa amesema ili kukakikisha linakuwa na kizazi chenye
maadili mema yatakayochangia maendeleo ya taifa na kwamba kila mzazi anatakiwa
kutimiza wajibu wake kwa kuwapa watoto wao malezi mema.
Askofu Dkt. Malasusa
amesema kila dini inassisitiza na kuhimiza kila mwenye mtoto kutoa malezi bora
yanayochangia ustawi wa jamii imara na taifa lenye maendeleo.
Amewasisitiza na
kuwahimiza viongozi wa madhehebu yote kuendelea kuwahamasisha waamini wao
kudumisha umoja, amani na mshikamano uliopo.
Mufti huyo amesema
hadi sasa Baraza la Waislamu Tanzania halijapata taarifa sahihi za watu
wanaotaka kwenda Hijja kutoka Wizara ya Hijja ya Saudia Arabia na Ubalozi wa
nchi hiyo nchini hivyo zikilifikia watatoa taarifa.
Naye Askofu wa
Kanisa la Menonite Tanzania, Dayosisi ya Masahariki na Pwani, Nelson Kisare
amesema waamini wa dini wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa kuendelea kuilinda nchi
hata baada ya kifo cha Rais Dkt. John Magufuli hivyo ni kuongozwa na Rais Samia
Suluhu Hassan ni jambo jema na la kihistoria kwa taifa.
Aidha, amesema jamii
inatakiwa kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto kwani ni dhambi na kusisitiza
elimu kutolewa kwa wahusika ili watambue madhara ya kukiuka haki za kundi hilo.
Askofu Mkuu wa Elimu
ya Pentekoste Peter Konki amekemea vitendo viovu ya kudhihaki Marais wastaafu
na aliyeoko madarakani kwa lugha ya matusi kwani kufanya hivyo kuwakosea
kulikosea taifa kwa ujumla.
Ameiomba Serikali
kushughulikia suala la mfumuko wa bei kwani linaathiri maisha ya watu wa
hali ya chini kwani wengi hushindwa kumudu gharama za maisha.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni