Zinazobamba

BISHOP LIPALA AWAPIGA MSASA MADEREVA WA BODABODA ZINGIZIWA, AWATAKA KUTII SHERIA ILI KUPUNGUZA AJARI BARABARANI

Bishop wa kanisa la Bethel Gospel Revival International Ministries (BIGRIM) Sebard Lipala akiwafanyia maombi madereva wa bodaboda wa kata ya Zingiziwa manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi kupitia jeshi la Polisi nchini imetakiwa kushirikiana na madereva wa bodaboda ili kuweza kuwasaidia kufuata sheria na kupunguza ajari zitokanazo na uzembe wa madereva hao.

Hayo yamesemwa mapema wiki hii na Askofu wa kanisa la Bethel Gospel Revival International Ministries (BIGRIM) Sebard Lipala wakati wa semina iliyandaliwa na kanisa hilo yenye lengo la kuwajengea uwezo madereva wa bodaboda wa kata ya Zingiziwa Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.

Askofu huyo amesema kuwa msukumo uliyomfanya aweze kuwakusanya madereva hao ni baada ya kuona ajiri nyingi zinazosababishwa na madereva hao na kuona kuna haja ya yeye kufanya jambo akiwa kama mtumishi wa mungu.

Ameongeza kuwa semina hiyo ilikuwa nzuri na vijana hao wa bodaboda wamefurahi sana kwa kuwa walikuwa wakidharaulika na kuonekana si kitu, lakini baada ya tukio hilo wamejiona ni watu wa thamani mbele za Mungu hata ndani jamii.

Aidha askofu huyo ameendelea kusema kwamba anatarajia kufanya kongamano kama hilo mwezi wa 12 mwaka huu, Na atawaongeza wataalamu mbalimbali ambao maswali yao hayakuweza kujibiwa kwenye semina hiyo, kama wataalamu wa Sayansi ya kijamii Pamoja na wahusikia wa mambo ya leseni Pamoja na vibari vya biashara.

Na mwisho amemaliza kwa kusema kuwa amewafanyia maombi maalum madereva hao ili waweze kupata pikipiki zao wenyewe kwa wasiyo nazo, lakini pia wenye mikataba wapate mikataba isiyokandamizi ili waweze kununua viwanja wajenge nyumba zao na kuachana na matumizi ya pesa yasiyo na maana bali wakomboe familia zao na kuisaidia serikali ka ujumla.

Afisa wa jeshi la Polisi kutoka kituo cha Polisi Chanika Inspector. Boniventure Bushumba akitoa elimu kwa madereva wa bodaboda kata ya Zingiziwa jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Muwezeshaji wa semina hiyo Inspekta Boniventure Bushumba kutoka kituo kidogo cha Polisi Chanika amempongeza Askofu Sebard kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuwakutanisha madereva hao na kuweza kuwapa elimu ya uzalendo kwa kuheshimu sheria za nchi ili kupunguza matukio mabaya ikiwemo ajari za barabarani.

Ameongezea kwa kuawataka madereva hao kuendelea kutii sheria bila shuruti ili wasiwaone askari polisi kama maadui zao kwani wakifuata sheria hakuna askari atakayewabuguzi katika majukumu yao ya kujitafutia riziki.

Na kwa upande wao madereva hao wa bodaboda wameahidi kuwa smart katika kazi zao pamoja na kufuata sheria zilizowekwa na nchi ikiwemo kuvaa vizuri pamoja na kuendesha pikipiki zao kwa weledi, Ili kupunguza matukioa ya ajari za barabarani.

Pia wameahidi na kuendelea kuwasihi wenzao ambao hawakuwepo katika mafunzo hayo kuacha kabisa vitendo viovu wawapo kazini na kusema kuwa watakwenda kuwafikishia elimu waliyoipata ili ajari zipungue ikiwezekana ziishe kabisa .   
Bishop wa kanisa la Bethel Gospel Revival International Ministries (BIGRIM) Sebard Lipala akiongea na vijana wa bodaboda kata ya Zingiziwa jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Madereva wa bodaboda wa kata ya Zingiziwa wakisikiliza kwa umakini elimu inayotolewa na viongozi mbalimbali.
Mwakilishi wa Diwani wa kata ya Zingiziwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Ngobedi Bw. Mohamedi Kirungi akitoa nasaha zake kwa madereva hao.
Baadhi ya washarika waliyoshiriki semina hiyo.

Boda boda zimepakiwa wenyewe wakiwa wanapatiwa semina ndani ya kanisa.

Bango la kanisa.

 

Hakuna maoni