Lema awa mkimbizi nchini Canada
Aliyekuwa mbunge wa
Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amehamia nchini Canada baada ya
kupata hadhi ya ukimbizi wa kisiasa akitokea Nairobi Kenya.
Hayo yameelezwa leo
Alhamisi Desemba 10, 2020 na katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani
Golugwa wakati akizungumza na Mwananchi Digital.
Wakati Golugwa akieleza
hayo, picha zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zinamuonyesha mbunge huyo
wa zamani akiwa kwenye ndege pamoja na mkewe, Neema na watoto wake watatu.
Novemba 8, 2020 Lema
alidaiwa kukamatwa akikimbilia nchini Kenya pamoja na familia yake kwa kile
alichoeleza ni kwa ajili ya usalama wake.
Gazeti la Standard la
Kenya liliripoti kuwa Lema aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini 2010 hadi 2020
alikamatwa Ilbissil Kaunti ya Kajiado baada ya yeye na familia yake kuvuka
kupitia mpaka wa Namanga.
Lema alikuwa ameondoka
nyumbani kwake kwa teksi akifuatana na mkewe na watoto wao watatu na kushuka
Namanga.
ADVERTISEMENT
Gazeti hilo linaeleza
kuwa Lema alisema mkewe aliwasilisha nyaraka kwa maofisa wa uhamiaji ambao
walikataa kuzitia mhuri na kutaka wafuatane na Lema.
Lema alinukuliwa na The
Standard akisema kuwa alikwenda ofisi za uhamiaji na hakuwa na hati ya
kusafiria na kwamba alikuwa anamsindikiza mkewe kwa ajili ya kutafuta shule kwa
ajili ya watoto wake.
Maofisa hao waliruhusu
familia hiyo kuvuka mpaka wakati Lema aliomba ruhusa ya kwenda kubadili fedha
za Kenya kumpa mkewe.
Mara tu alipovuka mpaka
aliingia kwenye gari la wakili wake, George Luchiri Wajackoyah ambaye baadaye
kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii alieleza kuwa Lema alikwenda Kenya
kwa ajili ya kulinda uhai wake.
Mbunge huyo alikamatwa na
polisi jijini Dar es Salaam Novemba Mosi, 2020 akiwa pamoja na mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe pamoja na aliyekuwa meya wa Ubungo, Boniface Jacob.
Polisi walieleza kuwa
watatu hao walikuwa katika kikao huku wakiwatuhumu kupanga mipango ya kufanya
maandamano yasiyo na kikomo kuanzia Novemba 2, 2020.
Maandamano hayo
yalitangazwa na Mbowe, kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto mKabwe
pamoja na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu lengo likiwa kushinikiza
uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020 urudiwe kwa kuwa haukuwa huru na wa haki.
Lema, Mbowe na Jacob
walipelekwa kituo cha polisi Oysterbay na kuachiwa kwa dhamana Novemba 3, 2020
huku wakitakiwa kuripoti kituoni kila watakapopangiwa

No comments
Post a Comment