Zinazobamba

WANAWAKE NCHINI WAPEWA ELIMU KUHUSU SARATANI KUTOKA LION KLABU,SOMA HAPO KUJUA


Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya TMJ, Dk.Walter Kweka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
WAKINA mama nchini wametakiwa kuwa na mwamko wa kwenda hospitali kila mwaka kufanyiwa uchunguzi wa Magonjwa ya Saratani hususani ya Shingo ya Kizazi kwani unapogundulika katika hatua za mapema unatibika.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya TMJ, Dk.Walter Kweka wakati akizunzungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la utoaji elimu na upimaji wa ugonjwa huo kwa walimu jijini hapa.

Zoezi hilo limelatibiwa na Lion Klabu ya Tanzania kwa kushirikiana na Hospiali ya TMJ 

“Watu watengeneze ule mwamko wa kwenda kuchunguza afya zao Kwa mfano unapozungumzia saratani ya matiti mtu yeyote ambaye anaona mabadiliko katika matiti, kwa mwananume na kwa mwanamke kwa sababu imezoeleka labda saratani ni ya akina mama tu ya matiti, na kwa wanaume pia inawakuta,”

“Kwa hiyo unapoona kuna tabia yoyote ya tofauti ndani ya kifua au matiti watu wawe na mwamko kwenda kuchunguza, tunapozungumzia saratani ya shingo ya kizazi wakina mama wawe na tabia yakufanya uchunguzi wa shingo ya kizazi kila mwaka kwa sababu tunapugundua tatizo mapema tunaweza kuwasaidia mapema.

Akizungumzia kuhusu elimu wanayo toa kwa walimu hao, Dk. Kweka amesema elimu hiyo itawaongezea ufahamu katika masuala ya saratani, ikiwemo ya shingo ya kizazi pamoja na saratani ya matiti na saratani nyingine.

Amesema lengo ni kwamba wanapojua waweze kujisaidia pamoja na kusaidia katika kuibua wagonjwa ambao wanakuwa na dalili za ugonjwa huo mapema katika jamii ili waweze kufika sehemu sahihi kwa ajili ya kufanya uchunguzi mapema kwani unapogundulika ukiwa kwenye hatua za awali unatibika.

Ameongeza kuwa wamechoka kupokea wagonjwa ambao wemekwishachelewa na mwisho wa siku mzigo kuwa kwa hospitali na madaktari kwa kushindwa kumsaidia.
Gavana wa Lion Klabu kwa nchi za Tanzania, Uganda na Sudani Kusini Rizwan Qadri akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kwa upende wake Gavana wa Lion Klabu kwa nchi za Tanzania, Uganda na Sudani Kusini Rizwan Qudri, amesema zoezi hilo linafanyika bure na ni zuri kwa ajili ya walimu hao  kuangalia afya zao dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

Amesema katika upimaji wa leo lengo ni kupima walimu 100 na kuele kuwa wanatarajia pia kufanya zoezi hilo katika maeneo mengine nchini.


Aidha amewataka watu wawe wanajitokeza kwa wingi inapotokea fursa kama hiyo ili waweze kuchunguza afya zao.
 Baadhi ya walimu wa jijini Dar es Salaam waliojitokeza katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya upimaji wa Saratani ya Shingo ya Kizazi na kupetiwa elimu juu ya ugonjwa huo.
Baadhi ya walimu wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya kupima Saratani ya Shingo ya Kizazi wakifuatilia kwa makini elimu juu ya ugonjwa huo ikitolewa na Dk. Walter Kweka (hayupo pichani.