Zinazobamba

JAMII YAOMBWA KUMPA NAFASI YA UONGOZI MTOTO WA KIKE ILI ATIMIZE NDOTO ZAKE

                   Jane Sembuche

Na Mussa Augustine.

Mkurugenzi Mkazi wa Plan International Tanzania Jane Sembuche ameiomba jamii kumpa nafasi mtoto wa kike katika kuwania nafasi za uongozi ili kuweza kutimiza ndoto zake za masuala ya uongozi.

Sembuche ametoa rai hiyo leo Oktoba 10, 2024 Jijini Dar es salaam kwenye hitimisho la kampeni ya chukua hatamu( Girls takeover) inayotekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania ,ambapo limehudhuriwa na wasichana wapatao 40 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

"Siku  yetu ya leo ambayo tunaiita Girls takeover au wasichana kushika hatamu ni kampeni ambayo Plan International kwa Tanzania na Nchi mbalimbali Duniani ambapo Plan ipo hua tunafanya kila mwaka ikiwa ni sambamba na kusherehekea siku ya watoto wa kike duniani ambayo hufanyika Oktoba 10,kila Mwaka" amesema.

Aidha amesema kuwa wasichana wanaweza kuwa viongozi wazuri katika jamii,nakwamba kitu cha msingi ni kuweka juhudi ,malengo na kujiamini yeye kama msichana anaweza kufikia malengo yake na anaweza kua kiongozi katika jamii na kuleta mabadiliko yanayotakiwa.

Akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba mwaka huu Mkurugenzi huyo Mkazi wa Plan International Tanzania amesema kuwa pamoja na shirika hilo kutekeleza Kampeni ya Girls takeover lakini pia lina kampeni nyingine ya "Sikia Sauti zetu " ili kuwezesha sauti za wasichana sehemu mbalimbali wanahamasika kuzungumza  nakuleta changamoto zao katika sehemu husika.

" Tunaamini wanaendelea kukuzika katika uongozi kuanzia ngazi za jamii na kupata uzoefu kwahiyo nikuhamasisha wote ambao wana uwezo wasifikirie kama kitu kigumu,wajitokeze kuwania nafasi hizo" amesisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi idara ya Maendeleo ya watoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu Bw.Mathias Haule amesema kuwa kampeni ya chukua hatamu(Girlstakeover) imeenda sambamba na kauli mbiu ya siku ya mtoto wa kike kimataifa inayosema "Mtoto wa kike na uongozi,tumshirikishe wakati ni sasa" ,hivyo Serikali kwa kushirikiana na Plan International itahakikisha watoto wa kike wanapata nafasi za uongozi katika maeneo mbalimbali hasa wakiwa mashuleni.

"Tunahamasisha watoto kuhamasisha wazazi wao kushiriki katika uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu unjao ,watoto wa kike wana nafasi kubwa ya uongozi ,na uongozi lazima ujifunze ,nakujifunza lazima itokane na watu wenye uzoefu" amesema.
                   Elizabeth Mafuru
Hata hivyo baadhi ya watoto wa kike akiwemo Elizabeth Mafuru anaesoma chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) nani Mkurugenzi Mtendaji wa (T-mark)ametoa wito kwa jamii kutoa nafasi kwa mwanamke kwamba anajua kuongoza na kuweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii.

Kauli ambayo imeungwa mkono na Felister Alex mwanafunzi wa UDSM ambaye alikua Balozi wa Norway kwa siku hiyo ambaye amesema amejifunza mengi ikiwemo kuwa kiongozi bora,mkakamavu na kujiamini hivyo jamii impe nafasi msichana ya uongozi katika jamii.


Hakuna maoni