Zinazobamba

DC. Batenga ampongeza Selemani Kaniki Kwa Kujenga Kituo Cha Polisi Chunya

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh. Mbaraka Alhaj Batenga ampongeza mdau wa Maendeleo Selemani Kaniki Kwa kujenga kituo kidogo Cha Polisi Kijiji Cha Ifumbo Wilayani Chunya.

Kituo hicho ambacho kitasaidia vijiji zaidi ya 10, ambapo hapo mwanzo hakukuwa na kituo cha Polisi kabisa.

Aidha Mh. Mbaraka Alhaj Batenga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya amewaomba wanakijiji hao kuweza kutunza kituo hiko na kuendelea kudumisha Amani ya nchi.

Mdau huyo wa Maendeleo Bw. Selemani Kaniki amukuwa akisaidia Kila Mkoa, Kila Wilaya na Kila Kata kote nchini Tanzania Kwa kuendelea kuun'ga Mkono juhudi za Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.


Hakuna maoni