KUELEKEA KWENYE MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KESHO,NECTA WATOA ONYO ILI KALI KWA WANAFUNZI NA WASIMAMIZI WA MTIHANI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Mtihani nchini,Dkt Charles Msonde |
NA KAROLI VINSENT
WAKATI wanafunzi wa kidato cha nne
wakitarajia kuanza kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne nchi kesho,Baraza la Mtihani nchini (NECTA)
limesema halitosita kumchukulia hatua mwanafunzi yeyote pamoja wasimizi wa
Mitihani hiyo ambao watajihusisha na vitendo vya udanganyifu kwenye mitihani
hiyo .
Pia,Baraza hilo limewapa onyo
wamiliki wa shule kuacha kuwaingilia
wasimamizi wa mitihani hiyo kwakuwa shule zao ni vituo maalum vya kufanyia
mtihani.
Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa
(NECTA),Dkt Charles Msonde wakati wa mkutano na waandishi,amesema Baraza hilo
linatoa wito kwa kwa wasimamizi wa
mitihani wote kufanya kazi yao kwa
umakini na uadilifu.
“Tunawaasa wasimamizi wa mitihani pamoja na wanafunzi kujiepesha na vitendo
vya udanganyifu kwani Baraza litachukua
hatua kali kwa yeyote yule
atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani ya Taifa”Amesema Dkt
Msonde.
Amesema Baraza hilo linawataka
wamiliki wa shule kutambua kuwa
shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo havitakiwi kuingilia majukumu ya
wasimamizi.
“Baraza halitasita kukifuta kituo
chochote cha Mitihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake wa
unahatarisha Usalama wa Mitihani ya Taifa”amesema Dkt Msonde.
Hata hivyo,Dkt amesema Baraza hilo linaamini kuwa walimu wamewaandaa vizuri wanafunzi hao
kwa kipindi cha miaka mine ya elimu ya sekondari hivyo hakutakuwepo na vitendo
vya udanganyifu.
Pamoja na hayo,Amesema katika mitihani huo Jumla ya watahiniwa 585,938
wamesajiliwa kufanya mtihani wa huo, ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni
323,513 na watahiniwa wa kutegemea ni 62,425.
“Kati ya watahiniwa wa shule 323,513 waliosajiliwa ,wanaume ni 159.103
sawa na asilimia 49.18 na wanawake ni 164,410 sawa na asilimia 50.82,huku
watahiniwa wenye uono hafifu ni 305 ambapo maandishi yao yanakuzwa”amesema Dkt
Msonde.
Kuhusu watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa ni 62,425 ,wanaume ni
28,574 sawa na asilimia 45.77 na
wanawake ni 33,851 sawa na asilimia 54.23 huku watahiniwa 6 wasioona.
Aidha,Baraza hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano katika
kuhakikisha mitihani hiyo ambayo inaanza kesho octoba 30 hadi 17 Novemba 2017 inafanyika kwa Amani na Utulivu
huku akiwaomba wananchi hao kuheshemu eneo la mtihani linapofanyika.