Zinazobamba

RAIS MAGUFULI ALISHAMBULIA VIBAYA GAZETI LA FREEMAN MBOWE,SOMA HAPO KUJUA


RAIS John Magufuli leo ametumia Dakika tano kulishambulia Gazeti la Tanzania Daima ambalo linamilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe, kwa kusema watu wa Gazeti hilo wamekosa Uzalendo na  nchi.

Rais Magufuli amesema kitendo cha Mwandishi wa Gazeti hilo na Mhariri wake kukubali kuchapisha habari ambayo inasema kuwa asilimia 67 ya watanzania wanatumia dawa za kupunguza  Makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV) , habari ya hiyoni ya kupika na yenye lengo ya kuichafua nchi.

Kauli hiyo ya Rais ameitoa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa Kamati ya Makinikia iliyofanikisha kufikiwa makubaliano ya kihistoria baina ya serikali na kampuni ya Barrick Gold yaliyofungua ukurasa mpya kwa Tanzania kunufaika zaidi na madini ya dhahabu.

Akizungumza kwa uchungu Rais Magufuli amesema alipokuwa anasoma  Gazeti hilo toleo la jana Jumapili tarehe 22/10/2017 ilikuwa na habari iliyokuwa ukrasa wa mbele yenye kichwa cha habari kuwa "Asilimia 67 ya watanzania wanatumia ARV"


Amesema alipoiona habari ile  alishtuka na kutaamaki.

"Jana niliposoma habari ile nikashtuka nikazani labda ilikosewa lakini nilipoangalia ukrasa wa tatu nikakuta hivyo hivyo,nikachukua simu na kumpigia waziri Afya nikamuuliza imekuwaje wakati unayasema haya mimi nilikuwa nakutazama na wewe hukusema haya imekuwaje tena,"

"Waziri Ummy akaniambi mimi sikusema hivyo ,kwani nilichosema mimi ni asilimia 67 ya watu wenye ugonjwa wa ukimwi ndio wanatumia Dawa za ARV,yaani katika watu elfu 5000 wenye virusi vya ukimwi ni asilia 67 tu ndio inatumia dawa hizo"

Rais Magufuli amesema kitendo cha watu hao kuruhusu habari hiyo ni ya kukosa uzalendo yenye lengo ya kuichafua nchi na kuwakatisha tamaa wawekezaji kuja kuwekeza.

"Leo hata kama mwekazaji anataka kuja kuwekeza lazima atashtuka na kuhofia kutokana na kuogopa kuwa asilimia 67 ya watanzania wanaugonjwa huu,ataogopa tu,:"