Zinazobamba

HAPATOSHI MAGUFULI NA ZITTO KABWE,, ZITTO AIBUKA NA KOMBORA HILI KWA SERIKALI YAKE,SOMA HAPO KUJUA


WAKATI leo Rais John Magufuli ni kama amempiga 'kijembe' cha kiana Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama Cha Act-Wazalendo ,Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli kutaka vyombo vya Dola kumchukulia hatua kwa kutoa takwimu za uongo kuhusu makusanyo ya kodi. 



Mbunge huyo ameibuka mda huu  ni Kombora jingine kwa Serikali ya Rais John Magufuli kwa kusema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya awamu ya tano imekopa dollar milioni 500 kutoka benki ya Uswiss na pesa hizo ndiyo zimetumika kulipa ndege za Tanzania.

Kabwe ambaye sasa anatajwa kuwa ni miongoni mwa  wakosoaji  wa serikali ya Magufuli  ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii .

Amesema kusema kuwa riba ya mkopo huo ni mkubwa sana na kudai watu wa chini wakiwepo wavuvi wa Migebuka. kutoka Kigoma watahusika kulipa deni hilo kupitia kodi zao.


"Serikali ya CCM ya awamu ya Tano imekopa $500m kutoka Benki ya Credit Suisse ya Uswiss Kwa riba kubwa Sana. Sehemu ya fedha hizo zimetumika kulipia ndege ambazo Serikali inanunua. Wavuvi wa Migebuka Kigoma watahusika kulipa deni hilo kupitia kodi zao" alisema Zitto Kabwe

Rais Magufuli leo amesema kuwa uchumi wa nchi unazidi kukuwa na kudai serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina pesa za kutosha ndiyo maana imeweza kununua ndege mpya zaidi ya sita kwa mara moja na kudai watu ambao wanasema uchumi umeshuka wanaichonganisha serikali na wananchi
.