Zinazobamba

KAMATAKAMATA YA VIGOGO WA CHADEMA YAREJEA TENA,,KIGOGO HUYU ANYIMWA DHAMANA,SOMA HAPO KUJUA

BENSON Kigaila, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema ametupwa rumande baada ya kukosa dhamana alipojisalimisha kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.
Kigaila aliitwa kwa mahojiano kwa tuhuma za kutoa lugha za kichochezi katika mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya Oktoba 12.
Frederick Kihwelo ambaye ni Mwanasheria wa Kigaila, amesema maamuzi juu ya dhamana ya mteja wake yataamuliwa kesho Jumanne.
”Polisi wamemhoji kwa masaa 3 kuanzia saa 7 hadi saa 10 na amehojiwa kwa makosa aliyoyafanya katika mkutano wake wa Oktoba 12 na wamekataa kutoa dhamana labda hadi kesho,” amesema Kihwelo.
KIhwelo ameongeza: ”Kimsingi makosa aanayotuhumiwa nayo yana dhamana, lakini wamesema wanaoweza kuamua ama kupata dhamana au kukosa hawapo ofisini.”
Mwanasheria huyo amesema katika mkutano huo Kigaila alizungumza mambo mengi ikiwamo kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kutekwa kwa Ben Saanane.
Kaimu kamanda wa kanda hiyo, Benedict Kitalika amesema upepelezi kwa sehemu kubwa umekamilika.