Zinazobamba

SERIKALI YA MAGUFULI KIBOKO,NDANI YA MIAKA MIWILI IMEYAFUNGIA MAGAZETI ZAIDI YA 400,AINGIA KWENYE REKODI YA KIPEKEE,SOMA HAPO KUJUA

SERIKALI ya Rais John Magufuli imeingia kwenye rekodi nchini. ya kuwa ndani ya kipindi cha Miaka miwili ya Utawala wake imeyafungia magazeti zaidi ya 400, na redoki hiyo inatajwa kuwa  haija wai kufanywa na watawala yeyote  tangia nchi kupata uhuru.Anaandika Karoli Vinsent Endelea nayo.

Rekodi hiyo inachagizwa leo baada ya serikali kutangaza kulifungia  Gazeti linalotoka kwa siku la Tanzania Daima, kwa siku Tisini baada ya kuandika wanayodai watawala hao ni ya uongo.

Kufungiwa kwa Gazeti hilo kuna kuja ikiwa ni ndani ya Miezi miwili serikali hiyo kutangaza kulifungia Magazeti yanayotoka kwa wiki mara moja  Mwanahalisi,Mawio,Raia Mwema kutokana na kudaiwa kuandika habari zinadaiwa ni za kichochezi.

Pia Serikali hiyo mwaka jana kupitia aliyekuwa waziri wa habari,utamaduni,sanaa na Michezo,Nape Nnauye alitangaza kuyafutia usajili  Magazeti 400 kutokana na kudaiwa magazeti hayo kutochapishwa kwa mda mrefu.

Akitangaza Uamuzi wa kulifungia Gazeti la Tanzania Daima leo Msemaji wa Serikali,Dkr Hassan Abasi alisema Gazeti hilo toleo la jumapili ya tarehe 21 /10.2017 lilandika habari yenye takwimu za uongo.

Katika toleo hilo Gazeti hilo lilisema "Asilimia 67 ya watanzania wanatumia dawa za kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi (ARV)
Katika habari hiyo ya Tanzania ilionekana kuichukiza serikali na kusababisha Rais John Magufuli kuzungumzia suala hilo alipokuwa akiwatunuku vyeti wajumbe wa kamati za madini Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais alisema habari hiyo ni mbaya kwa taifa kwa sababu inaweza kusababisha wawekezaji wasije kuwekeza nchini kutokana na kuhofia wapi wanaweza kupata wafanyakazi kwa sababu itaonekana Watanzania wengi wanaumwa.
Taarifa ya kuchukuliwa hatua kwa gazeti hilo imechapishwa na Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbasi.
Mmoja wa wahariri wa gazeti hilo, Saleh Mohammed amethibitisha kufungiwa gazeti hilo kwa muda wa siku 90.
Licha ya Gazeti hilo kuomba Radhi kupitia Toleo lake la jana Jumatatu ,lakini bado Serikali hiyo ikalifungia