Zinazobamba

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WAVIBANA VYOMBO VYA ULINZI,SOMA HAPO KUJUA

Kituo cha sheria na haki za binadamu lhrc kimeviomba vyombo vya ulinzi na usalama nchini  kuwachukulia hatua kali watu wote wanaoshiriki katika vitendo vya uhalifu.


Ombi hilo limetolewa jijini dar es salaam na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu dkt hellen kijo bisimba wakati akitoa tamko la maadhimsho ya siku ya amani duniani.
Dkt hellen amesema endapo vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya watu nchini vitafumbiwa macho vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
TAZAMA VIDEO KAMILI HIYO HAPO





B
Aidha bi kijo amewataka wananchi kutambua kwamba wao ndio walinzi wa kwanza wa amani nchini hivyo wanapaswa kufuata sheria na kuepuka vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.
Kila ifikapo septemba 21 dunia huadhimisha siku ya amani duniani ambapo kwa mara ya kwanza iliadhimishwa mwaka 1981 baada ya kuidhinishwa na mkutano mkuu wa umoja wa mataifa ikiwa na lengo la kuimarisha wazo la amani ndani ya baraza la umoja wa mataifa.

Kauli mbiu ya siku amani duniani kwa mwaka 2017 ni “pamoja kwa ajili ya amani, nidhamu, usalam na heshima kwa wote”