Zinazobamba

JAMAL MALINZI NA WENZAKE WAENDELEA KUSOTA RUMANDE,SOMA HAPO KUJUA

RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzanai (TFF) Jamal Malinzi na wenzake wanaendelea kusota rumande baada ya kesi yao kuahirishwa kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika.
Image result for jamali malinzi mahakamani
Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi October 5, 2017.

Mbali ya Malinzi, washitakiwa wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa Shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.