SAKATA LA SERIKALI YA JPM KUSEMA IPO TEYARI KUMTIBU LISSU,KAULI HIYO YAPINGWA KILA KONA,SOOMA HAPO KUJUA

SAA chache kupita baada ya serikali John Magufuli kupitia Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kusema ipo teyari kughalamia matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki,Tundu lissu,kwa ghalama yeyote endapo tu familia ya mbunge huyu ikihitaji.
Kauli hiyo ni kama imeibua majadala huku wengi wakiibinga,wa kwanza kuipinga ni Mbunge wa Tarime Vijijini,John Heche ameibuka na kumpinga waziri huyo kwa kusema wao wataendelea kuchangisha hela ya matibu kwa Lissu ambaye amelazwa Nairobi nchini kenya huku akihoji kuwa "toka lini matibabu ya mbunge yanaombwa na familia".
Heche ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii mara baada ya waziri Mwalimu kusisitiza Serikali inasubiri kupata maombi kutoka kwa familia ya mgonjwa ikiambatana na taarifa rasmi kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa”Serikali ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mhe.Lissu popote Duniani”.
Kauli hiyi ikamfanya Heche kusema haya
"Tangu lini familia ya Mbunge inatuma maombi serikalini kwenda kutibu mbunge anayeumwa?,watanzania tuendelee kumchangia lissu sisi wenyewe"amesema Heche kupitia mtandao huu wa Kijamii.
Kwa upande wake Mbunge wa Iringa Mjini,Mchungaji Peter Msigwa ameipinga hatua hiyo ya serikali kwa kusema serikali ya awamu ya tano inautani.
"Huu ni utani wa serikali ya awamu ya tano" amesema Peter Msigwa
Akizungumzai kauli ya serikali mchambuzi wa siasa kutoka Chuo Kikuu huria nchini,Ally Henga,Amesema kauli ya waziri haina mashiko kwani taratibu za kutibiwa mbunge ziko wazi.
"Hii ndio serikali ya matamko ndugu mtu akipewa nafasi ya kuongea anaongea anavyoweza,,jiulize huyu spika ndugai alipoumwa je ndugu waliomba akatibiwe au serikali ilichukua jukumu lenyewe,hawa wasitake siasa zao za majitaka,wameona wamepata aibu na dunia nzima imewaona ,leo wanakuja kujisafisha,mimi nawashauri wampuuze tu huyu waziri"amesema Henga