PLAN INTERNATIONAL YAKABIDHI KITUO CHA MALEZI AMBACHO KIMEGHARIMU 34,403,490 MKOANI GEITA
Turn off for: Swahili
Meneja
wa Plan Intarnational Mkoani Geita Gratian Mushema Kweyamba na Mgeni
Rasimi ambaye ni afisa ustawi wa jamii wilaya ya Geita Anderson Shimbi
wakizindua kituo cha malezi ya awali kwa watoto kwenye kijiji cha
Magenge.
|
Jiwe la msingi likiwa katika kituo cha malezi
|
Darasa la watoto kwaajili ya kujifunza mambo mbali mbali ambayo ni msingi wa maisha yao.
|
Bango linaloelekeza kituo kilipo.
|
Wananchi wakishuhudia tukio la uzinduzi wa kituo hicho.
|
Afisa mtedaji wa kata ya Magenge Julius Fumbuka akitoa utambulisho wakati wa hafra fupi ya uzinduzi wa kituo.
|
Meza kuu
|
Wananchi wakisikiliza kwa makini.
|
Meneja wa Plan Intarnational Mkoani Geita Gratian Mushema Kweyamba akielezea malengo ya mradi huo.
|
Msimamizi wa mradi huo Lydia Wanjala akitoa maelezo ya namna zoezi la mradio huo lilivyofanyika.
|
Afisa
mtendaji wa Kijiji cha Kaseme,Ndakilwa Ng'wanzalima akielezea namna
ambavyo kituo hicho kitakavyoleta faida kwa wananchi na watoto katika
kata hiyo.
|
Ukumbi wa mikutano kwaajili ya watoto.
|
Vifaa vya michezo mbali mbali.
|
Diwani wa kata ya Kaseme Andrea Kalamla ,akiomba ujenzi wa kituo hicho kujengwa pia kwenye kata yake.
|
Diwani wa kata ya Magenge,Edward Misungwi akihaidi kusimamia vikali kituo hicho.
|
Mgeni
Rasimi ambaye ni afisa ustawi wa jamii wilaya ya Geita Anderson
Shimbi,akisisitiza utunzaji wa vifaa vilivyopo kwenye kituo hicho.
|
Choo cha watoto.
|
vyoo vya walimu.
|
Picha ya pamoja .
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Shirika
lisilo la kiserikali la Plan International Mkoani Geita limekabidhi
kituo cha malezi na makuzi ya awali kwa watoto wadogo chenye thamani ya
sh,milioni thelathini na nne laki nne na elfu tatu mia nne na tisini
katika kata na kijiji cha Magenge wilayani hapa.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo na serikali ya kijiji,yaliyofanyika leo meneja
wa Plan Mkoani humo Gratian Mushema Kweyamba,alisema kuwa lengo la
ujenzi wa kituo hicho ni kumsaidia mtoto ambaye yupo chini ya umri wa
miaka sifuri hadi miaka mitano (5) ambapo anaweza kujifunza mambo
mbali mbali ya msingi.
“Tunaamini
kuwa kituo hiki kitawasaidia watoto kupata elimu ya kujitambua wakiwa
bado wadogo na ndio maana kauli mbiu yetu tunasema plan watoto kwanza,
tunaamini kuwa mtoto akijengewa misingi mizuri pamoja na malenzi
yaliyomema anaweza kuwa msaada kwa serikali na jamii
inayomzunguka”Alisema Kweyamba.
Akielezea
mafanikio ya ujenzi wa mradi huo,msimamizi wa kituo Bi,Lydia
Wanjala,amefafanua kuwa tangua waanze ujenzi wamefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kutokana na jamii ambayo ipo eneo husika kutoa ushirikiano kwa
kiasi kikubwa .
Akimwakilisha
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ,Afisa ustawi wa jamii ambaye ndiye
alikuwa mgeni rasmi kwenye makabidhiano hayo Anderson Shimbi
aliwashauri wanakijiji kuwa waangalizi wa mradi huo na kuutunza kwa
uangalizi mkubwa zaidi.
“Ndugu
zangu wanakijiji gharama iliyotolewa hapa ni kubwa sana hivyo
tunatakiwa sisi wenyewe tuwe watu wa kwanza katika utunzaji wa mali
hizi zilizopo kwenye kituo hiki”alisema Shimbi.
Diwani
wa kata ya Magenge,Edward Misungwi,ametoa ahadi ya kuhakikisha wanakuwa
walinzi wakubwa wa mradi huo na kwamba kwa mwananchi ambaye ataonekana
kukiuka masharti yaliyowekwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
|