Zinazobamba

MAKADA WA CCM WAJITOSA KUMTETEA RC MAKONDA,NI KUHUSU KASHFA YAKE YA KUIBA VYETI,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
WAKATI vyombo vya uteuzi ndani ya serikali  ya Rais John Magufuli. vikiwa kimya kwa kushindwa kujibu na kutolea ufafanuzi juu ya tuhuma zinazomkabili anayejiita na kuitwa Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuhusu kugushi vyeti vya kidato cha nne.

Makada mbali mbali wa Chama cha Mapindunzi (CCM) wameibuka na kuanza kumtetea mkuu huyo wa mkoa ambaye taarifa zinatajwa kuwa  amekimbilia nchini Afrika Kusini kwa mapumziko,kwa ajili ya kupisha uvumi unaoenea sasa.

Kwa kawaida,Watendaji wa CCM ambao wanakumbana na tuhuma mbali mbali zinazoibuliwa kwenye jamii,huwa mara kwa mara utumia baadhi ya makada wa chama hicho kuibuka na kuja kujitetea kuhusu tuhuma hizo na kuwasafisha ikiwemo kuiitisha mkutano na waandishi wa habari.

Methusela Gwajima ambaye amejitambulisha ni Mdogo wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat  Gwajima aibuka na kuitisha mkutano na waandishi wa habari katika hoteli moja iliyopo Magomeni Jijini Dar es Salaam na kumtetea Makonda huku akitoa mashambulizi kwa Askofu Gwajima ambaye ndio alioibua sakata la Makonda kughushi cheti.

Methusela ambaye pia amejitambulisha ni Wakali amesema watu wanahoji uhalali wa vyeti vya Makonda, wanataka kuzima Kashfa ya Kupambana na Madawa ya kulevya  aliyoidai imeibuliwa na Makonda.
Amesema kutokana na Madawa ya kulevya kuwaharibu vijana wengi nchini ameitaka jamii kupuuza suala la madai ya makonda kugushi vyeti badala yake amewataka kuendelea kumuunga mkono makonda kwa kile anachokiita “Vita ya Makonda ya Kupambana na Madawa ya Kulevya”
. “Wewe umeshatuhumiwa, umeitwa Polisi, hivi kwanini usisubiri uchunguzwe? Kama wewe huhusiki si utaambiwa basi. Wameitwa watu wengi, wameitikia wito, kwanini sasa yeye amegeuza kuwa ajenda? Mbaya zaidi imekuwa ni ajenda kanisani. Kwa hiyo kanisa limegeuzwa kuwa kijiwe cha siasa na watanzania wamekaa kimya hawasemi,” ameleza Methusela

"Kama Gwajima anadhani kuwa ameonewa aende mahakamani badala ya kukaa na kulalamika. Kwanini basi anakwepa mahakama na kufanya kanisa ndio sehemu ya kuzungumzia, kila Jumapili ni Makonda, Makonda, Makonda, vyeti, vyeti"  amehoji Methusela.

Mdogo huyo wa Gwajima bila ya kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kuonyesha juu ya ukweli wa taarifa za kufoji vyeti bali katika mkutano huo alijikita katika kumtetea Makonda na kusema wanaohoji kuhusu elimu ya Makonda ni wanatumiwa na wauza unga.
Makonda anayetetewa hapa,anatajwa kuitwa Daudi Bashite ambaye anatuhumiwa kubadilisha jina lake na kujiita Paul Christian ili aweze kujiunga na chuo baada ya kutajwa kufeli vibaya kwenye matokeo yake ya kidato cha nne.