Zinazobamba

KAMANDA MPINGA ASEMA AJALI ZA BARABARANI ZAPUNGUA,SOMA HAPO KUJUA

NA KAROLI VINSENT
JESHI la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani limesema matukoa ya ajali nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja yamepungua kwa asilimia 51 ikiwa tofauti na miaka ya nyuma.
Hayo yamelezwa hayo leo Jijini Dar es Salaam na Kamanda  wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchni ,Naibu Kamishna Muhamedi Mpinga wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya “Abilia Paza Sauti” Kampeni hiyo ilikuwa na lengo la kutoa elimu kwa Abilia pamoja na madereva ili waweze kuzifahamu sheria mbali  mbali za barabarani kwa lengo la kupunguza Ajali nchini.
Mpinga amesema Jeshi hilo kwa kushirikiana na Asasi mbali mbali za kiserikali na zisizokiserikali ambazo wamezitumia  kutoa elimu kwa madereva na Abilia kumechangia kupungaza ajali ambazo zilikuwa zinatokana na uzembe kwa madereva.

Akitoa Takwimu hizo,amesema kwa kipindi kama hiki kwa mwezi wa pili kwa mwaka huu kumetokea ajali 453 ambapo kipindi kama hiki kwa mwaka jana kumetokea ajali 846 jambo analodai kupungua kiwango hiki hakijawai tokea katika kipindi cha hivi karibuni.
Naye Mratibu wa Kampeni hiyo,John Sika amesema katikakampuni hiyo iliyodumu kwa miezi sita wamefanikiwa kutoa elimu kwa wananchi takribani elfu sitini pamoja na madereva elfu sita.
Amebainisha kuwa Kampeni hiyo,imesaidia kwa kiwango kikubwa katika kupunguza ajali nchini ambazo amedai zimekuwa zikichangiwa kwa waendeshaji vyombo vya moto na abalia kutokuwa na elimu ya usalama barabarani.