WAZIRI MAHIGA AWAGEUKA WATANZANIA WALIOFUKUZWA MSUMBIJI,SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa
Watanzania waliokuwa nchini Msumbiji wamefukuzwa kutokana na kukiuka taratibu
na sheria za kuishi nchini humo na akataka suala hilo lisiharibu mahusiano
mapana yaliyopo ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar
es Salaam, Balozi Mahiga alisema Tanzania imekuwa na ushirikiano na Msumbiji
kwa muda mrefu hivyo utaratibu walioufuta wa kuwaondoa wahamiaji hao ni wa
kiuungwana.
Alisema jana mawaziri wa nchi 14 walianza kuwasili
nchini kwa ajili ya kikao cha mawaziri ambacho Tanzania ni mwenyekiti wao, na
siyo kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya Msumbiji, ila yenyewe ni nchi jirani
na watazungumzia masuala ya ulinzi na usalma na ushirikiano wa nchi hizi za
SADC.
Alisema watu hao ambao waliingia Msumbiji bila
kufuata taratibu, wakiwa huko pia wamevunja sheria za nchi hiyo kwa kujihusisha
shughuli bila vibali na kinyume cha taratibu za ajira za nchi hiyo sanjali na
kujiingiza katika vitendo vya uhalifu mbaya.
“Watu hawa wanajihusisha na biashara za madawa ya
kulevya, silaha na wanapokonya ajira za watu wa nchi hiyo... wahamiaji hao siyo
Watanzania pekee, bali na nchi zingine. Lililowagusa zaidi eneo hilo lina
madini na linafanana na Mererani na wameanza kufanya biashara hizo kinyume cha
Sheria na wameona raia wa Msumbiji hawanufaiki na biashara hiyo,” alieleza.