TUNDU LISSU AIUMIZA KICHWA SERIKALI,BAADA YA KUGOMBEA TLS,SOMA HAPO KUJUA
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA), Tundu Lissu, amesema ameanza kuogopwa na viongozi wa
serikali baada ya jina lake kuwa miongoni mwa majina matano bora ya
wagombea wa nafasi ya urais katika Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
kutokana na misimamo yake ya kuitetea Katiba ya Tanzania.
Akizumgumza na waandishi wa habari Mwanza
jana, Lissu alisema tangu atangaze nia yake ya kugombea urais wa TLS
ameanza kuogopwa kutokana na kujulikana kwa misimamo
yake kuhusu masuala ya sheria, siasa na katiba ya
nchi hii.
Alisema TLS ina majukumu makubwa katika nchi ya
kulinda utawala wa sheria na wanasheria ndiyo wanaojua kuliko mtu yeyote
zinapotungwa sheria mbovu na zile za kikandamizaji, pia wao ndiyo wanapaswa
kuwa wa kwanza kuanza kuzipigia kelele sheria hizo.
“Kwa miaka mingi TLS imeongozwa na watu
ambao hawafikiri kwamba wajibu wao wa kwanza kulinda utawala wa sheria,
wao wanafikiri wajibu wao wa kwanza ni kuwapendeza wanasiasa na matokeo
yake TLS imepotea, wanachoogopa ni kwamba hii raha ambayo wameipata miaka
yote hii wakati wanasheria wa TLS wakiwa usingizini akija
huyu Lissu itaisha,” alisema Lissu.
Alisema aligombea nafasi hiyo baada ya
kumsikia Rais Dk. John Magufuli akizungumza mbele ya watanzania kwamba
wakili yeyote atakayewatetea watuhumiwa wanaokutwa na
dawa ya kulevya au nyara za serikali wakamatwe na kuwekwa ndani.
Alisema aliposikia kauli hiyo alicheka na kusema
sasa ni wakati wa yeye kuwa rais wa TLS ili kauli za aina hiyo zikome na siku
mbili kabla ya Rais Dk. John Magufuli kutoa kauli hiyo, Bunge lilipitisha
sheria ya msaada wa sheria.
“Sheria hiyo inasema mtu yeyote anayefunguliwa kesi
ya jinai, au madai kama ni maskini hana uwezo wa kumlipa wakili atapatiwa
huduma hiyo na wakili atalipwa na mtendaji mkuu wa mahakama.
“Sheria hiyo inampatia haki mwananchi yeyote
atakayekuwa na kesi ya mauaji, pembe za ndovu au dawa za kulevya
kupata wakili atakayelipwa na serikali.
“Siku mbili baadaye Rais anakinzana na sheria hiyo
nilishangaa kweli. Tayari sheria hiyo imetungwa ni jambo muhimu
kweli kwa sababu katika nchi hii watu wanasingiziwa sana, kwenye
magereza nyingi nchini wamejazana wananchi ambao hawana hatia na
wapo huko kwa sababu hawakuwa na mawakili wa kuwatetea,” alisema Lissu.
Lissu alisema endapo atachaguliwa kuwa rais wa
TLS atahakikisha sheria ya msaada wa sheria inatekelezwa.
Kuhusu hoja ya Waziri wa katiba na
Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ya kutishia kukifuta chama hicho hicho kwa kuwa
kimeanza kujiingiza katika masuala ya siasa, Lissu alisema wanaoleta hoja za
kutaka kukifuta chama hicho kama ni wanasheria ujuzi wao wa sheria ni wa shaka
lakini kama ni wasiojua sheria wanasamehewa.
Alisema sheria ya iliyoanzisha TLS inasema
mwanachama yeyote aliyekidhi vigezo vya chama hicho ana haki ya kuwa
mgombea wa nafasi yoyote ya uongozi na haijasema ukiwa mwanachama wa
chama chochote cha siasa unapungukiwa sifa ya kugombea.
“Watu wanazungumza kana kwamba ni makosa
mwanasheria kuwa mwanasiasa, katika nchi hii katiba imeruhusu siasa za
vyama vingi, kuwa wanachamaau kiongozi wa chama.
“Kuwa tu mwanachama una kuwa na fursa ya kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi serikalini lakini sasa watu wanataka kuaminishwa
kuwa ukiwa mwanasiasa huna haki,” alisema