Zinazobamba

TANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA MBOLEA DUNIANI OKTOBA 13 MWAKA HUU MKOANI MANYARA.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti  wa Mbolea Tanzania ( TFRA) Joel Laurent.

Na Mussa Augustine.

Tanzania inatarajia kuungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Mbolea Duniani itakayofanyika Oktoba 13 ,2024 ambapo kwa mara ya kwanza siku hii iliadhimishwa Nchini Uingereza Mwaka 2016.

Kwa upande wa  Tanzania Maadhimisho hayo yameadhimishwa mara sita ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika Mkoani Katavi Mwaka 2019,nakwamba kwa Mwaka huu yatafanyika Mkoani Manyara kuanzia Oktoba 10 hadi 13 ,2024 na yatafunguliwa na Mkuu wa Mkoa huo Mh.Queen Sendiga na siku ya kilele mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Kilimo Mh.Hussein Bashe.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 1,2024 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti  wa Mbolea Tanzania ( TFRA) Bw.Joel Laurent wakati akizungumza na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ,kuelekea maadhimisho hayo.

Amesema kwamba maadhimisho hayo ni mpango wa Kimataifa unaoungwa mkono na Jumuiya za tasnia ya Mbolea Duniani kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu faida na matumizi sahihi ya Mbolea na kuchochea juhudi za ubunifu katika teknolojia za Kilimo kwa mustakabali wa Maendeleo endelevu ya usalama wa Chakula.

Amesema kwamba katika maadhimisho hayo wataalamu mbalimbali kutoka Taasisi za utafiti,Kampuni za Mbolea,vyuo vikuu,Mashirika yasiyo ya Kiserikali na wadau wa Kilimo watapata fursa ya kutoa Elimu kwa wakulima ikiwemo Elimu ya matumizi sahihi ya Mbolea,matumizi ya mbegu Bora na udhibiti wa Tasnia ya Mbolea kwa ujumla.

" Kuanzia tarehe 8 hadi 12 wakulima watapata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika mashamba ya mfano yaliyoandaliwa na Mamlaka ambapo wataona tofauti bayana kati ya mazao yaliyotumia Mbolea na Yale ambayo hayajatumia Mbolea na hivyo Kuwapa hamasa au ushawishi wa kutumia Mbolea ili kuongeza tija katika uzalishaji" amesema

Nakuongeza kuwa" kwa mwaka huu 2024 kauli mbiu ya Siku ya Mbolea Duniani inasema" Tuongee Mbolea,Kilimo ni Mbolea," lengo ni kuonesha umuhimu wa Mbolea kama kichocheo Cha uzalishaji wa mazao ya Chakula, Biashara,mboga mboga,na matunda ,ambapo ukuaji wa tasnia ya Mbolea unaendelea kuchochea Kilimo Biashara kutokana na ongezeko la matumizi sahihi ya Mbolea.

Aidha Mkurugenzi Mkuu huyo wa TFRA ameendelea kufafanua kuwa kauli mbiu hiyo inaenda sambamba na juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuthamini umuhimu wa Mbolea katika Sekta ya Kilimo ambapo kwa misimu mitatu mfululizo Serikali imeendelea kuwanufaisha Wakulima kwa kuweka Ruzuku kwenye Mbolea mbango ambao umeongeza hamasa ya matumizi ya Mbolea kwa Wakulima na kuchochea na kuongeza tija katika uzalishaji.

"Kwa Mwaka huu mamlaka (TFRA) imeandaa Kongamano la aina yake la Kimataifa la Kwanza la Mbolea litakalofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma Oktoba 11 na 12 ,Kongamano hilo litawakutanisha pamoja Wadau wa tasnia ya Mbolea Kitaifa na Kimataifa ,linatarajiwa kuja na majibu ya changamoto zinazoikabili tasnia ya Mbolea na wakulima kwa ujumla,ambapo mgeni rasmi katika Kongamano hilo atakua Katibu Mkuu wa Wizara y Kilimo ndugu Gerald Mweli" amesema.

Nakuongeza kuwa mada zitakazojadiliwa kwenye Kongamano hilo litakalohudhuriwa na washiriki wapatao 250 kutoka ndani na nje ya nchi , ni pamoja na Usimamizi thabiti wa Mbolea,Tathmini ya mifumo na udhibiti Bora wa Mbolea,mchango wa Afya ya udongo katika kusimamia  usalama wa Chakula Nchini.

Mada zingine ni matumizi ya Tehama katika kusimaia Tasnia ya Mbolea,kuhamasisha uzalishaji wa ndani ,matumizi sahihi ya Mbolea na Biashara ya Mbolea katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusaini mwa Afrika ( SADC)

Aidha amesema kwamba Jioni ya tarehe 11 ,Oktoba 2024 Waziri wa Kilimo ,Mh.Hussein Bashe atazindua Mkakati wa Maendeleo ya Tasnia ya Mbolea Nchini Tanzania.
                    Bw.Louis Kasera
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya ruzuku Taifa TFRA, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi uzalishaji wa ndani na ununuzi wa Mbolea kwa pamoja Bw.Louis Kasera amesema kuwa kwa sasa matumizi ya Mbolea yamefikia kiasi cha tani laki nane na arobaini kwa mwaka ukilinganisha na tani laki tatu na sitini Mwaka 2021/2022 kipindi ambacho mpango wa utoaji wa Mbolea ya ruzuku ukianzishwa na Rais Dkt Samia.

"Matumizi ya Mbolea yamepanda kutokana na wakulima wengi kuanza kuhamasiaka kutumia Mbolea ya ruzuku  kwa usahihi zaidi katika maeneo mbalimbali Nchini.

Aidha amesema kuwa Mamlaka hiyo imefanikiwa kudhibiti Mbolea feki kutokana na matumizi ya mfumo wa kidigitali ambapo wamekua wakifuatilia taarifa zote ambako mkulima amepitia kupata Mbolea hiyo ,hali ambayo inasaidia kuwatambua kwa urahisi wasambazaji wa Mbolea feki


Hakuna maoni