Zinazobamba

MKUU WA WILAYA KINONDONI AWA MBOGO,AWASHUKIA WATENDAJI SOMA HAPO KUJUA



Ally Hapi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akitoa maagizo kwa watendaji wa kata wakati akiwa kwenye ziara ya siku kumi

NA KAROLI VINSENT
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi amewashukia Maafisa utendaji wa serikali wa kata wa manispaa hiyo kuwa  hatosita kuwachukulia hatua Kali watendaji hao, pale endapo  kutakapobanika kwenye maeneo yao kuna mgonjwa wa kipindupindu.

Pia,Hapi amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Aroni Kagulumjuli,kuwaandikia barua maafisa hao watendaji ,kuwachukulia hatua kai wananchi wote ambao watashindwa kuwalipia gharama za usafi ili waweze kufikishwa mahakamani.

Mkuu Huyo wa wilaya ametoa maagizo hayo Leo wakati alipokuwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya siku 10, katika kata zote zilizopo Ndani ya wilaya hiyo ,ambapo ziara hiyo yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Amesema kwa sasa atamfumbia macho Maafisa watendaji wa Kata wakiwemo,Afisa Afya,Afya elimu ambao wanajukumu la  kusimamia usafi kwenye maeneo yao endapo wakishindwa kusimamia jukumu hilo na kupelekea mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu.

Amesema ugonjwa wa kipindupindu unatokana na uchafu hivyo amedai yeye atakubali kadhia hiyo ya ugonjwa utokee maeneo hayo.

Agizo hilo la Hapi limekuja baada ya Afisa Mtendaji wa kata Mzimuni,Shabani Kambi baada ya kumwambia mkuu huyo  kuwa wameshindwa kukusanya uchafu kwa wakazi hao kutokana na wananchi kushindwa kutoa tozo ya ubebaji taka kila mwisho ya Mwezi.

Ndipo Hapi akamtaka Mkugenzi wa Manispaa kuwaandikia barua watendaji wa wote wa manispaa hiyo kuwakamata  wananchi na kuwafikisha mahakama ya Jiji wachukuliwe hatua Kali za kisheria,amedai kuwa serikali haitoweza kuwavumilia wananchi ambao wanazalisha uchafu wakitegemea serikali igaramie kutoa uchafu.

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akizungumza na Wafanyabiashara wa soko la magomeni,leo wakati wa muendelezo wa ziara ya siku 10 katika kata zote za manispaa hiyo
Katika hatua nyingine Hapi ametembelea Soko la Magomeni kujionea hali soko,alitembelea shule za kata ya mzimuni pamoja na mradi wa maji,na badae alifanya mkutano wa wazi kwa wakazi wa kata ya mzimuni ambapo alisikiliza kero mbali mbali.