TEACHERS JUNCTION YAWATAKA WALIMU KUTOJUTIA KUSOMEA UALIMU
![]() |
Mtoa mada akifafanua jambo wakati Teachers Junction walipotembelea chuo cha ualimu Vikindu |
Taasisi ya kuongeza thamani ya mwalimu TEACHERS JUNCTION
imewataka walimu kutojutia kusomea ualimu kwakua endapo atajilaumu
hatoweza kuwa na hamasa ya kufundisha vizuri wanafunzi darasani.
Akizungumza wakati wa semina fupi kwa wanalimu watarajiwa
katika chuo cha ualimu Vikindu mkoani pwani,Afisa miradi wa TEACHERS
JUNCTION bwana NJAWA SALUMU amesema Taasisi yao ipo kwa lengo la kumpa
thamani mwalimu yoyote nchini hasa kwa kumtafutia eneo analolitaka
kufanyia kazi hasa katika shule binafsi endapo atakuwa na vigezo bila
kuzunguka na bahasha mwalimu huyo kutafuta kazi.
Afisa miradi huyo bwana SALUMU ameongeza kuwa endapo
mwalimu atakuwa ameipenda taaluma yake ya ualimu itakuwa rahisi
kutafutea kila kona na shule binafsi kwakua na.uwezo mkubwa katika
taaluma yake na kufanya kushinda soko huria la ualimu.
Kwa Upande wa mmiliki wa shule ya sekondari ya Mwandege
Boys bwana ENOCK MRISHA amewaeleza walimu hao watarajiwa kuwa waajiri
wengi wanakuwa na wasiwasi sana walimu wazuri kuibiwa ,hivyo
amefananisha na wale walimu wenye uwezo mdogo kuhofia kufukuza kazi muda
wote hivyo amewataka kujianda vyema kushindana na soko huria.
Hata hivyo taasisi inayoongeza thamani kwa walimu TEACHERS
JUNCTION kwa kushirikiana na wamiliki wa shule binafsi wametoa wito kwa
walimu wote kupenda taaluma yao na TEACHERS JUNCTION itawasaidia kufanya
kazi na shule binafsi hapa nchini.