RC MAKONDA AZIDI WEKWA MTU KATI,ULIMWENGU AJITOSA NAYE KWENYE VITA ,SOMA HAPO KUJUA
Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu, leo
anatarajia kuwasilisha maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
akiomba kuungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika kesi ya
katiba iliyofunguliwa hivi karibuni.
Ulimwengu anaomba kuunganishwa katika kesi ya katiba
namba 1 ya 2017 kama mdai dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na
Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
“Maombi ya kumuunganisha yameandaliwa na
kesho(leo) yatakuwa mahakamani kuomba naye awe mdai. Anaomba kujiunga kwa kuwa
mambo anayopigania Mbowe naye ana maslahi nayo kwa sababu ni mambo muhimu ya
katiba,” alisema mmoja wa jopo la Mawakili kutoka Kurugenzi
ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya Chadema, Peter Kibatala.
Katika kesi hiyo ya katiba, Mbowe anaomba Mahakama
Kuu itamke kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha na
kukamata.
Mbowe pia anaomba mahakama itengue vifungu vya 5
&7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki ya
katiba.
Mbowe alifungua kesi hiyo akidai Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda amekiuka sheria na taratibu katika kushughulikia
watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya nchini.
Kesi hiyo ya katiba inasikilizwa na majaji watatu,
Jaji Sakieti Kihiyo, Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Khaday.
Baada ya kufungua kesi hiyo Mbowe pia aliomba
mahakama itoe amri asikamatwe mpaka maombi yake ya zuio yatakaposikilizwa na
kutolewa uamuzi.
Mahakama ilitoa zuio la muda kwa Jeshi la
Polisi kutomkamata Mbowe hadi maombi yake ya kupinga kukamatwa
aliyowasilisha mahakamani yatakaposikilizwa.
Maombi hayo yalitakiwa kusikilizwa mwishoni mwa wiki
lakini upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Gabriel Malata
uliwasilisha pingamizi, ukiomba mahakama iyatupilie mbali kwa sababu hana
msingi katika sheria.
Upande wa mdai ulijibu hoja za kupinga maombi yao na
Mahakama ilisikiliza hoja za pande zote mbili na kupanga kutoa uamuzi wa
pingamizi hilo Machi 2, mwaka hu