Zinazobamba

DC HAPI ATANGAZA VITA NA WAVAMIZI WA ARDHI KINONDONI,SOMA HAPO KUJUA


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi aliyevaa koti akiwa na watendaji mbali mbali wa mitaa wakati akiwa kwenye ziara katika kata ya Wazo,ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku kumi kukagua miradi ya maendeleo kwenye kata zote zilizopo kwenye Wilaya yake pamoja na kusikirika kero za wananchi
NA KAROLI VINSENT
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, ametangazia vita kwa watu wote  wale waliovamia  maeneo  ya wazi,ikiwemo na wale watu waliojimilikisha maeneo  kinyume na taratibu  katika  Manispaa hiyo, atahakikisha maeneo hayo yanarudishwa  na wavamizi hao kichukuliwa hatua.

Hapi ametangaza vita hiyo Leo  wakati alipokuwa kwenye ziara  katika kata ya wazo ikiwa na mwendelezo wa ziara ya siku kumi kwenye kata Zote zilizopo kwenye Manispaa hiyo kwa Lengo la kukagua Miradi ya Maendeleo na kusikiriza Kero za wananchi.

Amesema katika Wilaya yake kuna tatizo Kubwa la uvamizi wa maeneo ya wazi na  watu Kujimilikisha na kuweka makazi bila kufuata taratibu  na  kupelekea kuchangia kuibuka migogoro.

"Yaani katika Wilaya yangu tatizo la uvamizi wa maeneo ya wazi limekuwa kubwa Sana,yaani majambazi wanatoka kona mbali mbali za dar es salaam wanakuja kuvamia Kinondoni hususani kata ya wazo,na kupelekea migogoro ya ardhi na mimi sitokubali"amesema Hapi.

Hapi Amesema atatumia nguvu zote kuhakikisha maeneo hayo yanarudishwa sehemu husika huku akiviagiza vyombo vya ulinzi kushirikiana na watumishi wa Halmashauri kuhakikisha wanawakamata watu hao na kuwafikisha mahakamani.

Sanjari na hilo,Pia Hapi Amepiga marafuku umiriki wa Mashamba ndani ya Manispaa hiyo kwa madai kuwa inachangia kuleta vurugu kutokana na wananchi hao kushindwa kuyaendeleza maeneo hayo na kupeleka wavamizi kuvamia shamba.

"Nawaomba watendaji wa Manispaa Mpo hapa mnanisikiliza sitaki kuona umiriki wa shamba kwenye halmashauri yangu,hawa ni tatizo,hivyo nataka wenye mashamba haya vi vipimwe  ili view viwanja "ameelekeza, Hapi.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya, amewasihi Mwenyeviti wote wa serikali za mitaa kwenye halmashauri hiyo kuhimiza wananchi wachangie tozo ya ukusanyaji taka,hivyo akawataka kutosita kuwachukulia hatua watakaidi agizo hilo.