SIMBA YAIBAMIZA YANGA TAIFA LEO,SOMA HAPO KUJUA
Klabu ya Yanga ilianza vyema mchezo ndani ya dakika
za mwanzo kabisa na kupelekea mchezaji Obrey Chirwa mwenye jezi namba 7
mgongoni kufanyiwa madhambi ndani ya kumi na nane na mchezaji wa Simba Novat
Lufunga na kupelekea Yanga kupata penati ndani ya ya dakika 4 za mchezo na
kupigwa vyema na mchezaji Simon Msuva wa Yanga.
Yanga iliendelea kuongoza kwa bao hilo la kwanza
huku wakiwa na moto wa kutafuta goli la pili, katika dakika ya 23 Yanga
walipata kona ya kwanza ambayo ilipigwa na mchezaji Haruna Niyonzima lakini
kipa wa Simba aliweza kuicheza vyema na kuondoa hatari ya Yanga kupata goli la
pili ndani ya dakika za mwanzo mwanzo.
Kocha wa Simba Omug alipoona kikosi chake hakina
mwenendo mzuri ndani ya dakika 27 alimtoa Luizio na kumuingiza Said Ndemla
ambapo hapo kidogo mchezo kwa upande wa Simba ulibadilika na kuanza kufanya
mashambulizi, huku wakijaribu
Ndani ya dakika 32 Goli kipa wa Yanga Deogratius
Munishi alidaka mpira na kukaa nao kwa muda na kupeleka faulo ambayo ilipigwa
na Said Ndemla wa Simba lakini Ndemla alikosa na kupoteza nafasi ya kusawazisha
goli la kwanza.
Yanga iliendelea kufanya vyema na kujaribu mara
kadhaa katika lango la Simba bila mafanikio, ndani ya dakika 43 Simba
ilibahatika kupata faulo nyingine tena ambayo ilipigwa na mchezaji Ajib lakini
mpira huo ulikwenda nje.
Mchezo uliendelea kwa kasi na mashambulio kwa timu
zote mbili, na ilipofika dakika ya 47 mchezaji wa Yanga Thabani Kamusoko
alitoka nje baada ya kupata majeraha na kuingia Said Juma Makapu.
Mpaka muda wa mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa
bao moja dhidi ya Simba huku ikiwa imetawala mchezo kwa asilimia 51 na Simba
ikitawala mchezo kwa asilimia 41.
Baada ya kurudi kwa kipindi cha pili timu zote mbili
zilikuwa na hamasa ya mchezo na ushindi hamasa hizo zilipelekea mchezaji wa
Yanga, Endrew Vicenti alipata kadi ya njano ndani ya dakika 56 mchezaji wa
Simba alipigwa kadi nyekundu na kutoka nje ya uwanja na kuwaacha Simba wakiwa
pungufu uwanjani.
Katika kipindi cha pili baada ya kuingia mchezaji
Kichuya Simba ilibadilika na kuanza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na
kuonyesha uwezo katika kucheza mpira jambo lililopelekea mchezaji Mavugo wa
Simba ndani ya dakika 66 kupata goli la kwanza kwa Simba na kuweza kusawazisha
na kuwa bao moja kwa moja.
Mpka dakika ya themanini ya mchezo Simba kupitia kwa
mchezaji wake Shiza Ramadhan Kichuya aliiandikia Simba goli la pili dhidi ya
Yanga huku timu hiyo ikiwa pungufu uwanjani.
Mpaka mpira umekwisha Simba 2-1 Yanga (Mavugo 66,
Kichuya 81 : Msuva 5)