PIGO KWA MILLARD AYO,MICHUZI.BLOG,GLOBAL TV .SERIKALI YAPIGA MARUFUKU HUDUMA ZAO,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Ankal Issa
Michuzi wa Michuzi TV, Millard Ayo na Askofu wa Ayo TV na Abdallah Mrisho wa
Global TV wakitoka makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano walikoitwa kuchukua
barua zao zinazowazuia kuendelea kutoa huduma za TV mtandao hadi hapo kanuni za
usajili na leseni utapokamilika.
|
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV, AYO TV na Global TV
kusitisha huduma zao za TV mtandaoni hadi hapo kanuni za usajili rasmi ambazo
mamlaka hiyo imesema inaandaa kwa huduma hizo zitapokuwa tayari.
Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James
Kilaba tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa sana nchini na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.

"Kwa
mujibu wa section 13 (1) of the electronic and
postal communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma zozote za aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano", imesema barua hiyo.
Wamiliki wa mitandao hiyo - Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi
na Abdallah Mrisho - wameeleza kushtushwa kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati hata kanuni zenyewe hazijawekwa.
"Gloval TV ipo tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili - kama zingekuwepo – na kwa sababu bado kukamilika tunaomba kupewa muda zaidi chini ya uangalizi wakati tunasubiria kanuni hizo mpya," alisema Abdallah Mrisho, Meneja Mkuu wa
Global Publishers.
Ankal Michuzi na Millard Ayo waliunga mkono kauli hiyo na kwa pamoja watatu hao wameomba kuonana na mkurugenzi wa TCRA ili kuwasilisha maombi rasmi ya kuruhisiwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wakati kanuni zikisubiriwa.
Bahati mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa kushughuliwa ataporejea wiki ijayo.
"Ukizingatia kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na haijulikani kanuni zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya kufanya ili wananchi wanaotutegemea sana wasikose huduma hii", alisema Ankal. Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mchakato wa TV mtandao.