MSANII UWOYA KUANZISHA KANISA LAKE NA KUWA MCHUNGAJI,SOMA HAPO KUJUA
Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema kuwa ana mpango
wa kuwa Mchungaji pamoja na kumiliki kanisa lake yeye mwenyewe siku za usoni na
kwamba anamuomba Mungu kila siku aweze kutimiza ndoto hizo.
Kauli hii imetoka kinywani mwa msanii huyo pindi
alipokuwa akijibu maswali mubashara aliyokuwa anaulizwa na mashabiki zake
kupitia katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipindi cha Kikaangoni
"Nina ndoto ya kuwa mchungaji na kila siku huwa
nina muomba Mungu anifanikishie suala hilo niweze kutimiza japokuwa sasa hivi
bado nipo katika changamoto kubwa ila natumai ndoto zangu zitatimia. Natamani
kuwa pastor ambaye ni mwalimu, niwafundishe watu Mungu anataka nini, lakini
sitaki kuanzisha kanisa kama biashara, sitaki kucheza na Mungu, ndiyo maana
najipanga kwanza sitaki kukurupuka, nataka niwafundishe watu Mungu anataka
nini, na jinsi ya kumuomba Mungu". Alisema Uwoya
Uwoya pia amefunguka na kueleza kuwa kazi yake ya
sanaa huwa inamtesa kiimani jambo ambalo linamfanya kila siku akiamka awe
anatubu kwa ajili ya mambo anayoyafanya akiwa katika kazi zake za uigizaji .
Amesema katika tasnia ya uigizaji mara nyingi huwa
wanaongea uongo na hata mambo mengi wanayoyafanya kufikisha ujumbe huwa ni vitu
ambavyo havimpendezi Mungu.
"Mimi nina hofu ya Mungu sana pia napenda
kusali linapokuja suala la kazi yangu ukweli naona kama inanisumbua imani yangu
kwa sababu katika uigizaji mambo mengi tunayoyafanya siyo ya kumpndeza Mungu
lakini ndiyo kazi sasa, kila siku asubuhi nikiamka huwa inabidi kumuomba
msamaha mungu wangu ndiyo niendelee na kazi". Amesema Irene Uwoya.
Kwa waliotaka kujua kama Irene anatumia dawa za
kulevya, amewajibu kuwa hatumii dawa za kulevya na hajawahi kutumia kwa kuwa ni
mkristo na dini yake hairuhusu kutumia dawa za kulevya wala kushiriki katika
ndoa za jinsia moja lakini pombe anakunywa
"Situmii dawa za kulevya lakini nakunywa bia,
dini yangu haizuii kunywa, nina uwezo wa kumaliza hata kreti nzima, hata
mapadre kwenye dini yetu wanakunywa, lakini hairuhusiwi kulewa"
Pia amefunguka kuhusu mapenzi yake ya kuvaa nguo
fupi, ambapo amesema anapeda nguo fupi, kwa kuwa ana mzio 'allergy' na nguo
ndefu, hivyo hawezi kuvaa nguo ndefu.