CCM YANGUKIA PUA KESI YA UBUNGE,SOMA HAPO KUJUA
CC
Mahakama ya Rufani Kanda ya Arusha leo imetupilia
mbali rufani ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Longido Onesmo Ole Nangole
(Chadema), baada ya kukiuka amri ya Mahakama hiyo iliyomtaka afanye marekebisho
kwa kuandika upya rufani yake.
Akisoma uamuzi wa Mahakama, Msajili wa Mahakama ya
Rufani Tanzania, Amir Msumi, amesema, Ole Nagole alikiuka amri ya Mahakama
iliyotolewa Oktoba 24, mwaka jana iliyomtaka aongeze majina ya Msimamizi wa
Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika rufani yake mpya kabla ya kesi
kusikilizwa..
Mh. Jaji Msumi amesema Mahakama imeridhishwa na
pingamizi lililowasilishwa na upande wa Mjibu Rufani, Dk. Masumbuko Lamwai,
(CCM), aliyetaka rufani hiyo isisikilizwe kwa madai imeandikwa upya bila idhini
ya Mahakama.
Matokeo ya Ubunge wa Onesmo Ole Nangole yalitenguliwa
Juni 29 mwaka jana, kwa madai kulikuwa na dosari nyingi ikiwemo kujazwa matokeo
ya Ubunge kwa kutumia fomu namba 21c za kujaza matokeo ya udiwani na kujaza
matokeo ya Ubunge, badala ya kutumia fomu namba 21b.
Ole Nangole alikuwa akipinga kutenguliwa kwa matokeo
hayo ambapo alikuwa akipambana na mgombea wa CCM Dk, Steven Kiruswa