Zinazobamba

KUHAMA KWA WIZARA KWENDA DODOMA KWA SHIKA KASI,WIZARA HII NAYO KWAHERI DAR ES SALAAM,SOMA HAPO KUJUA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisini kwake Mjini Dodoma. Waziri Mahiga leo ameutangazi Umma wa Watanzania kuwa Wizara imehamia rasmi Dodoma.


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017. Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, Awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28 Januari, 2017 na Awamu ya Pili imetekelezwa tarehe 17 Februari, 2017. 

Miongoni mwa Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza (Awamu ndogo ya kwanza tarehe 28 Januari, 2017) nipamoja na Viongozi Wakuu na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P.Mahiga na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10) waliofuatana nao. Awamu ndogo ya kwanza ilifuatiwa na (Awamu ndogo ya Pili tarehe, 17 Februari, 2017) iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P.Mlima na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M.Mwinyi wa kiongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Katika Uhamisho huo wa Awamu ya Kwanza, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi wao Wakuu.

Mawasiliano ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa nikama ifuatavyo:

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Barabara ya Makole,

S.L.P 2933,
Jengo la LAPF, Ghorofaya6,

DODOMA
Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,

Nukushi : +255-26-2323208,

Barua pepe : nje@nje.go.tz Tovuti : www.foreign.go.tz

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dodoma, 27 Februari, 2017