Zinazobamba

KESI YA MSANII WEMA YAAHIRISHWA,MASOGANGE NAYE PANDISHWA MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA



Mwigizaji Wema Sepetu leo alienda tena  Mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana kwenye sakata la dawa za kulevya baada ya kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi  15 March 2017 baada ya upande wa Mashtaka kusema upelelezi bado  haujakamilika 


 
NAYE MREMBO WA VIDEO MASOGANGE KESI YAKE YAWA HIVI.
Msanii  Agnes Gerald 'Masogange' amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka ya kutumia dawa za kulevya.

Mrembo huyo ambaye ni maarufu kwa kupamba video za muziki wa wasanii wa bongo fleva, amekana tuhuma hizo na kesi yake kuahirishwa hadi Machi 2i mwaka huu.

Katika mashtaka yake mawili yaliyosomwa na mwendesha mashtaka Mashauri Wilboard chini ya wakili wa serikali Constatine Kokulwa, Agnes anadaiwa kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepan kwa nyakati tofauti.

Mara baada ya kusomewa mashtaka yake, ameachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 10.

Pia mrembo huyo ambaye amewahi kukamatwa nchini Afrika Kusini akihusishwa na usafirishaji wa dawa za kulevya, ametakiwa kutotoka nje ya Dar es Salaam kwa kipindi chote cha kesi bila kibali cha mahakama.