Zinazobamba

BREAKING NEWS,YUSUFU MANJI HALI YAKE YAWA MBAYA NDANI YA SELO ALIPO,SOMA HAPO KUJUA

HALI ya Mwenyekiti wa Klabu ya Mpira ya Yanga,mfanyabiashara Yusufu Manji yawa mbaya zaidi baada kutolewa Kituo cha Polisi cha kati Jijini dare s Salaam anakoshikiliwa na kukimbizwa Hispitalini.
Kwa mujibu wa Vyanzo vya karibu vilivyo kwenye kituo hicho, kinasema majira ya jioni hii ,gari la kubeba wagonjwa lilionekana kituoni hapo huku akitolewa Manji kutoka ndani ya kituo hicho cha polisi na kupakiwa kwenye gari la wagonjwa teyari kwa kukimbizwa Hospitali.

Fullhabari.blog ilimtafuta Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Siiro  kuzungumzia hali hiyo,simu yake haikuweza kupatikana.

Mfanyabiasha Manji anashikiliwa na Polisi tangu Alhamisi ya wiki iliyopita baada ya kutii agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda aliyemtaja Manji na pamoja na watu wenginge 64 ambao wanatajwa kuhusika katika kuuza Madawa ya kuleva.