Zinazobamba

WATENDAJI WA MAGUFULI WAANZA KUMLUKA MAGUFULI MWENYEWE,AGIZO LAKE KWA MACHINGA LAGEUKWA,SOMA HAPO KUJUA




Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga katika maeneo ya soko la Kariakoo na barabarani, hususan karibu na barabara za mabasi ya mwendo kasi.

Akizungumza jana na Kamati ya Bunge, Waziri huyo wa TAMISEMI alisema kuwa kurejea kwa wafanyabiashara hao katika maeneo hayo kumeleta usumbufu mkubwa na uchafu wa mazingira katika maeneo ya jiji.

“Namuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaondoe na asilegeze kamba,” alisema Waziri Simbachawene.

Alisema kuwa hali hiyo imetokana na tafsiri isiyo sahihi ya agizo la Rais John Magufuli alipokuwa ziarani Mkoani Mwanza.


“Wala agizo  la Mheshimiwa Rais halikumaanisha hicho. Mheshimiwa Rais alisema tuwatafutie maeneo mbadala ambao wapo maeneo kama ya Mwanza na walikuwa wanafanya biashara ya kuuza nguo, akizungumzia wale particular group walioko pale Mwanza. Kwa Dar es Salaam tulishamaliza huko,” alisema.

Aidha, alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha hakuna hata machinga mmoja atakayeonekana akifanya biashara katika maeneo ya barabara za mabasi yaendayo kasi.

Aigizo hilo la Waziri Simbachawene liliungwa Mkono na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge ambao walisema kuwa hali ya soko la Kariakoo imekuwa mbaya kutokana na kuzagaa kwa machinga.