WAKILI KIBATALA NAYE KAMA TUNDU LISSU AIBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Wakili Peter Kibatala |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa uamuzi wa hoja zilizokuwa
zikibishaniwa na mawakili wa pande mbili katika kesi ya uchochezi inayomkabili
Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anaandika Faki Sosi.
Hoja zilizotolewa na upande wa
mashtaka wakati kesi hiyo ilipotajwa kwa mara ya kwanza, ya kwamba wakili Peter
Kibatala hana uhalali wa kumtetea Lissu katika kesi hiyo kutokana na kuwa ni
mmoja wa mashahidi wa upande wa Jamuhuri, ilikuwa ikitolewa uamuzi.
Cyprian Mkeha, Hakimu Mfawidhi katika mahakama hiyo
ametoa uamuzi wa shauri hilo kwa kutupilia mbali hoja za upande wa mashitaka.
Hakimu Mkeha, amesema kuwa, hakuna sheria yoyote
inayomzuia Kibatala kumtetea mteja wake kama upande wa mashitaka ulivyodai na
hivyo ataendelea kumtetea Lissu.
Baada ya uamuzi huo kutolewa, kesi hiyo itatajwa
tena tarehe 19 Septemba mwaka huu.
