TGNP WATAJA SABABU ZA WANAWAKE KUSHINDWA KUCHOMOZA KATIKA MEDANI ZA KISIASA
Hayo yamebainika katika kongamano maalum lilolenga kuwajengea uwezo Wanawake ili waweze kupambana na changamoto zinakwamisha jitihada za wanawake kuchomoza katika nafasi mbalimbali za Uongozi hapa nchini.
Katika Kongamano hilo lililohudhuriwa na aliyekuwa Spika mstaafu
ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama ANNA MAKINDA, Wanawake walibainisha vikwazo mbalimbali wanavyokumbana navyo wakati wa kusaka nafasi za uongozi, lakini kubwa wakisisitiza juu ya suala la umasikini na Rushwa ya Ngono.
Kwa muda mrefu wanaharakati wa
haki za wanawake na wadau mbalimbali wameendelea kupambana kuhakikisha kuwa
wanawake wanapata nafasi sawa katika Nyanja mbalimbali ikiwemo ya
uongozi lakini jitihada hizo zinaonekana kukwamishwa na Umasikini.
Kongamano hilo Liliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP
kwa kushirikiana na ACTIONAID mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake
hao kupambana katika nafasi mbali mbali za uongozi nchini.
| Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo Spika mstaafu Mama Anna Makinda akiwa katika Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa wanawake |
Aidha wameeleza kuwa
kwa uzoefu walioupitia katika uchaguzi wa mwaka jana imeeonyesha kuwa Rushwa ya ngono ilikuwepo kwa kiasi cha
kuwakwamisha baadhi ya wanawake na wengine kuogopa kujitokeza katika nafasi
hizo huku pia familia zikishindwa kuwaunga mkono wanawake wanaotaka kugombea
kwa kile walichoita ni kuogopa aibu ya rushwa ya ngono kwa familia.
| Wanawake mbalimbali wakichangia mijadala katika shughuli hiyo |
Wanawake hao ambao walikutana
kwa mara ya kwanza Mjini Dodoma mwaka 2015 kabla ya uchaguzi mkuu na baaadae
kukutana Wiki hii kupeana mrejesho wa kile kilichotokea katika uchaguzi mkuu wa
mwaka jana wamesema kuwa wanaitaka serikali Asasi za kiraia,TAKUKURU na wadau
wengine kuongeza jitihada za kukemea Rushwa ya ngono na kuongeza uhamasishaji
ili iweze kuzunguziwa kwa uwazi ili kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria
katika kulishughulikia Tatizo hilo.
Aidha wanawake hao
wameitaka serikali kurekebisha sheria ya usajili wa vyama vya siasa ya mwaka
1992 itamke rasmi uwiano na usawa wa kijinsia katika nafasi kuu za maamuzi
ndani ya vyama na pia sheria ivitake vyama vya siasa kuteua wanawake asilimia
50 kwenye kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za vijiji hadi Taifa.