Zinazobamba

Serengeti Boys yaweka rekodi ya kutofungwa mechi 11 mfululizo

Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imeandika historia mpya hapa nchini baada ya kufanikiwa kuandikisha rekodi ya kucheza michezo 11 mfululizo ya kimataifa bila ya kupoteza. 


Wachezaji wa Serengeti Boys baada ya moja ya vipindi vya mazoezi yao. ( Picha Soka360 )
Wachezaji wa Serengeti Boys baada ya moja ya vipindi vya mazoezi yao.
Katika mechi za kimataifa Serengeti Boys imecheza dhidi ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia (2) na Marekani, Shelisheli ( 2) na Madagascar.
ilianza kwa kuifunga Misri mabao 2-1 katika uwanja wa Taifa na kufanikiwa kuifunga tena 3-2 katika uwanja wa Chamazi siku tatu baadae.
Baada ya hapo Serengeti Boys ikaalikwa katika michuano maalum nchini India.
Katika mashindano ya AIFF nchini India,  Serengeti Boys iliyokuwa timu pekee kutoka Afrika  ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goa ilicheza na timu ambazo ziko juu  katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
Ilianza michuano ya AIFF kwa kutoa sare ya mabao 1-1 na Marekani kisha ikawachapa wenyeji India kwa mabao 3-1. Ikafuatiwa na sare ya 2-2 na Korea Kusini.
Sare nyingine ya mabao 2-2 dhidi ya Malaysia ikafuatiwa kabla ya kuichapa Malaysia mabao 3-0 katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
Kisha ikacheza mechi mbili dhidi ya Shelisheli katika mbio za kuwania kufuzu kwa fainali za vijana za mataifa ya Afrika na kushinda nyumbani na ugenini kwa jumla ya mabao 9-0.
Leo ikatimiza sare ya
Kabla ya kuanzakuchezamechi za kimataifatimuhiyoilichezamichezokadhaa ya ndani na timu za chini ya vijana na kupotezamchezommoja tu dhidi ya Alliance Academy.
Jumamosi ijayo Serengeti Boys itaivaa Afrika Kusini katika hatua ya pili ya mchujo wa kuwania kufuzu kwa fainali za vijana kwa mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Madagascar.