Zinazobamba

RC MAKONDA ATEKELEZA AHADI YAKE KWA WAISLAM,SOMA HAPO KUJUA

Agosti 15 Mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alionyesha dhamira yake ya kutaka kujenga Ofisi za Makao Makuu ya Baraza la Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA), baada ya kukabidhi ramani ya jengo la ofisi hizo kwa Muft Mkuu wa Tanzania Abubakari Zuberi na kuhaidi kukamilika kwa jengo hilo ndani ya miezi 14, ambapo zilizuka hoja kuwa hatoweza kutekeleza kwa kuwa amahaidi mengi na hajayatekeleza kikamilifu.MAKONDA BAKWATA LEO (8)

Akizungumza jijini Dar es Salaam zilizopo ofisi hizo za BAKWATA Makonda ameeleza kuwa wanaopinga jitihada zake wanawivu usiokuwa na tija kwani yeye ni kiongozi wa watu wote wa Mkoa wa Dar es Salaam bila kujali dini, rangi, jinsia, kabila na itikadi za kisiasa, hivyo atahakikisha wote wanapata haki sawa lakini ameamua kuanza na viongozi wa dini kwa kuwa wanastahili kuenziwa, kuheshimiwa kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ya kulinda, kuombea amani na kuwa amrisha mema waumini wao.BAKWATA NEW

Huku akieleza kuwa katika jitihada hizo za ujenzi wa ofisi za BAKWATA, amepata ufadhili kutoka Taasisi ya GSM Foundation ambao watalijenga jengo hilo la ghorofa tatu litakalo gharimu Shilingi Bilioni 5 na milioni 200, kwa muda wa miezi 14 kama alivyo agiza Mkuu wa Mkoa Makonda wakija na ramani tofauti na jengo lililokusudiwa awali, huku likiwa na nguzo tano kama ilivyo Dini hiyo ya Kiislamu, Ukumbi wa Mikutano, Maktaba, Kompyuta,lifti, ofisi za kisasa za Mufti zikiwa nne katika ghorofa ya tatu na ofisi nyingine ya Sheikh Mkuu wa Mkoa, Katibu Mkuu wa BAKWATA,Kadhi, Baraza la Maulamaa, kumbi za wanawake.MAKONDA BAKWATA LEO (2)