RC MAKONDA AMPONDA KIKWETE,SOMA HAPO KUJUA

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ni
bora kuliko serikali ya awamu ya nne, anaandika Faki Sosi.
Makonda ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika
utawala wa awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amesema serikali
iliyopita ilikuwa na matabaka kati ya viongozi na wananchi tofauti na ilivyo
sasa.
Makonda alikuwa
akizungumza leo katika kipindi cha Terminal cha Clouds Fm leo alasiri.
“Serikali ya
sasa inafanya kazi nzuri zaidi. Kuna tofauti kubwa kati ya ya watawala na
viongozi kwa sababu kiongozi anasifa ya kuwasikiliza anaowaongoza lakini
mtawala hana sifa hiyo,” amesema Makonda.
Amejinasibu kuwa
Mkoa wake wa Dar es Salaam umekuwa Mkoa wa kipekee kwani viongozi
wanashirikiana na wananchi moja kwa moja.