Zinazobamba

MFUMO WA ELIMU WA SASA UBADILISHWE,RODRIGUZ WA UN ATOA USHAURI WA SERIKALI YA JPM,SOMA HAPO KUJUA


Pichani nI Mwakilishi wa  Umoja wa Mataifa kwa upande wa Tanzania  Alvaro Rodriguz (picha na Maktaba)



NA KAROLI VINSENT
SERIKALI nchini imetakiwa kubadilisha mfumo wa elimu ya sasa ambao umebainika unamwandaa mhitimu kutegemea ajira na  kwenda kwenye mfumo wa elimu unaomwandaa mhitimu kujitengenezea ajira na kuwa mbunifu.

Imeelezwa njia hiyo italisadia taifa ambapo katika kipindi hichi cha serikali  ikitarajia kuwekeza zaidi kwenye Viwanda..

Ushauri huo umetolewa na Mwakilishi wa  Umoja wa Mataifa kwa upande wa Tanzania  Alvaro Rodriguz wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari wenye lengo la kumwaga  Mwakilishi mkazi wa umoja wa Taifa ambalo linashughulikia idadi ya watu UNFPA, Dr Natalia Kanen ambaye amechanguliwa kuwa Naibu Katibu mkuu  kwa upande wa Dunia
,

Rodriguz amesema kwa sasa Tanzania kila mwaka vyuo vyake inazalisha wasomi wanaomaliza Chuo kikuu wanaofikia milioni 1 huku wengi wao wakikosa ajira.
Amesema Njia sahihi ya kuweza kuwasaidia watu hao ni kwa serikali kubidilisha mfumo wa elimu wa sasa na kuupeleka kwenye mfumo wa elimu utakaoweza kuwajengea wahitimu kuwa wabunifu.
Kwa Upande wake,Naibu Katibu mkuu mpya,Dr Kanen amewapongeza viongozi wa Tanzania kwa kufanya nae kazi kwa ushirikiano kwa zaidi ya miaka miwili aliyokuwa hapa nchini.
Amesema Ushirikiano aliopata hapa Tanzania umepelekea hadi kuchaguliwa kushika nafasi.huku akiwahasa Watanzania kuhakikisha wanamuinia mtoto wa kike kwa kumpatia elimu ambayo amedai itaweza kumkomboa na kulileta taifa maendeleo.