Zinazobamba

TIGO, MILVIK WAJA NA BIMA MKONONI MWAKO...SASA WATEJA WAKE KUFURAHIA BIMA YA KULAZWA

 Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitangaza ushirikiano kati yao na Tigo kutoa bima watakayoimudu watanzania. Kutoka kushoto ni Meneja wa Promosheni wa Tigo, Mary Rutta, Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel na Meneja Maendeleo ya Biashara wa Resolution Insurance, Zamaradi Mbega.


KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Milvik Tanzania pamoja na Kampuni ya bima ya Resolution imekuja na huduma mpya ya Bima Mkononi, huduma ambayo inamuwezesha mteja wa Tigo kuweza kurejeshewa gharama za matibabu mara tu anapopata matatizo ya ugonjwa.

Akitangaza kuzinduliwa kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin alisema,Huduma hiyo itasaidia wateja wa Kampuni ya Tigo kutokuwa na wasiwasi mara wanapopata matatizo ya kiafya kwani Tigo imezamiria kurudisha gharama zake ndani ya siku tatu mara baada ya kupokea maelezo ya mteja.
 Pia amesema huduma hiyo itasaidia kuziba pengo  kati ya wateja  na hivyo kuongeza  upenyezaji wa huduma hiyo kwa njia ya simu katika maeneo ya mjini na vijijini nchini Tanzania, tunaamini Bima Mkononi  itakuwa ni kicdhocheo kikubwa  cha kusukuma ujumuishwaji wa  huduma za fedha  katika sekta isiyo rasmi kwa kuwawezesha Watanzania kuzifikia huduma za bima  wanazozimudu kutoka kwenye simu zao.” 

"Tunawaomba watanzania kuchangamkia huduma hii ya Bima Mkononi kwani haina gharama kubwa kama bima zingine na kwamba uhakika wa kurudishiwa gharama zako ni wa hali ya juu". Alisema
 Akifafanua kuhusu huduma hiyo, Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo,Ruan Swanepoel alisema, “Kuzinduliwa kwa huduma hii  kupo kwenye mikakati ya Tigo ya kuboresha mageuzo katika mfumo wa maisha ya kidijitali na katika kuongoza kwake  katika kutoa teknolojia ya kisasa  na ubunifu  kwa kuwezesha huduma ya Bima Mkononi kufikiwa kupitia Tigo Pesa.”

 Amesema Mteja yeyote wa Tigo anastahili kujiunga na huduma ya Bima Mkononi, Kiingilio cha awali  2,999 ambayo itadumu kwa miezi miwili, 7,999 yenyewe itadumu kwa miezi 6 na bima ya Shilingi 15,999 itakayodumu kwa miezi 13 ambapo mteja katika huduma hiyo anapata bima ya ajali ya Mil.1.2 kwa mwaka.

Akizungumzia kwa nini bima ya kulazwa, amesema bima hiyo ni nzuri kwa ulinzi wa familia kutokana na hatari za kifedha zinaoweza kuikabili familia yako. kwa kiasi kidogo cha Sh. 2999 mteja anaweza kupata fidia ya Tsh.40,000 kwa siku hadi Tsh. Mil. 1.2 kwa mwaka
  Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel (wa pili kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
 Meneja wa Promosheni wa Tigo, Mary Rutta akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu bima hiyo.
 Meneja Maendeleo ya Biashara wa Resolution Insurance, Zamaradi Mbega (kulia), akizungumzia mpango huo wa bima.



Hakuna maoni