EPZA YAJIVUNIA KUWEZESHA WATANZANIA KUPATA AJIRA...YASISITIZA ILI UCHUMI UKUE LAZIMA BIDHAA ZIUZWE NJE YA NCHI
Ofisa Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Nakadongo Fares (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka hiyo. Kushoto ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge.
Zaidi ya ajira rasmi 36,000 na zisizo rasmi 300,000 zimeweza kutengenezwa kwa Watanzania kutokana na makampuni zaidi ya 140 kuwekeza katika Mamlka ya maeneo maalum ya uzalishaji kwa mauzo ya nje yaaani EPZA
Akizungumza
na Waandishi wa habari, Ofisa Muhamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka hiyo,
Nakadongo Fares amesema mpaka sasa ajira nyingi zimeweza kutengenezwa
na wanaonufaika zaidi ni Watanzania.
Ameyasema hayo katika maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Alisema kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuhasisha uwekezaji katika kanda maalumu za kiuchumi, kuvutia na kuhamasisha uhuishaji wa teknolojia mpya, kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda usindikikaji wa malighafi zinazopatikana nchini, kutengeneza fursa za ajira na kuongeza pato la fedha za kigeni nchi.

Naye Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge amesema dhumuni kubwa la Mamlka hiyo ni kuhamasisha uwekezaji katika kanda maalum za Kiuchumi na kwamba sasa wamewekeza zaidi katika kuhamasisha sekta binafsi kushiriki shughuli za namna hiyo.
Akizungumzia hali ya uelewa kwa sekta Binafsi kuingia katika mfumo wa EPZA, Lemunge amesema tayari wameanza kuona matunda kwani kuna watu wameanza kujitokeza kushirriki.
Ametaja moja ya Kampuni ambayo imeanza kuchukua hatua ni Star infrastructure development T Limited ambayo imekuja na mradi wa Star city Launch utakaotekelezwa huko Morogoro.
Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na wanahabari.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Star Infrastructure Development (T) Limited, Ananth Bhat akizungumzia mradi wao wa uwekezaji uliopo mkoani Morogoro.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni