Zinazobamba

SHIRIKA LA MADINI (STAMICO) LAJIPANGA KUJENGA VITUO SITA VYA ELIMU

 Ofisa Matukio ya Dharura wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Jeremia Ibambasi (kulia), akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo mara baada ya kuonyesha kwa vitendo jinsi zoezi la uokoaji linavyyofanywa katika machimbo
 
 
Imeelezwa kuwa Shirika la madini la Taifa (STAMICO) limedhamilia kujenga vituo sita katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambayo kwa muda mrefu kuna machimbo ya madini, dhamira ikiwa ni kutoa elimu kwa wachimbaji wadogowadogo waweze kufanya kazi zao kwa weledi wa hali ya juu.
 
Hayo yamebainishwa leo katika mkutano maalum na waandishi wa habari, uliofanyika katika banda la nishati na madini viwanja vya sabasaba.
 
Amesema kuanzishwa kwa vitu hivyo vitakuwa msaada mkubwa wa kutoa elimu kwa wachimbaji wadowadogo  ambao hakika wanastahili kujengewa uwezo.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo (kulia), akiangalia waokoaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) jinsi wanavyomsaidia  mtu aliyevuta hewa chafu kwenye kiwanda cha uchanjuaji dhahabu nje ya banda la Wizara ya Nishati na Madini katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016 katika viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo mchana.
 Hapa mfanyakazi wa Stamico, Paul Thobias (katikati), akionesha jinsi anavyosaidiwa na wataalamu baada ya kuvuta hewa chafu kiwandani.
 Zoezi la kumtoa nguo majeruhi likiendelea. Nguo hizo zinahisiwa huwenda zikawa na hewa hiyo ya sumu.
 Majeruhi akiendelea kutolewa nguo.
 Wananchi wakifuatilia zoezi hilo kwa karibu huku wengine wakiwa wameshika tama.
 Waokoaji wakiondoka na majeruhi wakimpeleka lilipo gari la kubebea wagonjwa tayari kumpeleka mgonjwa Hospitali.
 Hapa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na maofisa mbalimbali wa wizara yake baada ya kwisha kwa zoezi hilo la uokoaji.
 Hapa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na maofisa mbalimbali wa wizara yake baada ya kwisha kwa zoezi hilo la uokoaji.
 Hapa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na Ofisa wa Matukio ya Dharura wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Jeremia Ibambasi.

Hakuna maoni