TAARIFA MUHIMU KUTOKA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU,SOMA HAPO KUJUA
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Jerry Sabi (katikati) akiongea na waandishi wa
habari wa vyombo mbalimbali na kutoa taarifa ya awali ya zoezi la kuhakiki
wanafunzi wanufaika wa mikopo ya wanafunzi lililoanza Mei 30, 2016 na
linaloendelea katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
|
WANAFUNZI 2,739 hawakujitokeza kuhakikiwa katika zoezi la uhakiki wa wanafunzi kwenye Taasisi za elimu ya juu nchini lilifanywa na Timu maalum iliypoundwa na Bodi ya Mikopo kuanzia tarehe 30 Mei, 2016 ambapo hadi sasa zoezi hilo linaendelea.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Jerry Sabi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa Katika zoezi la uhakiki wa wanafunzi jumla ya taasisi 26 zimehakikiwa, ambapo uchambuzi wa taasisi 18 umekamilika.
Amesema zoezi la kuhakiki wanafunzi linaendelea katika vyuo mbalimbali hapa nchini wataza na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yosefu, Chuo cha Biashara – Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Chuo Kikuu cha Mwenge, Chuo cha Biashara - Dodoma na Chuo Kikuu cha Ushirika - Moshi.
Pia Bodi ya Mikopo imetoa wito kwa wanafunzi wote ambao hawajahakikiwa kujitokeza haraka ili wahakikiwe kabla ya kuhitimisha zoezi hilo.