SAKATA LA KUFUNGIWA DK MWAKA,LAZIDI KUCHUKUA SURA MPYA,SHIVYATIATA WAIBUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO
Pichani ni Dk Mwaka |
SIKU chache kupita baada Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia wazee na Watoto,kupitia Baraza
la tiba asili kuvifutia usajili wa kituo cha Fore plan cha Dk Juma Mwaka na vingine viwili. kwa kile
wanachodai vituo hivyo vikiuka kanuni ya Tiba asili.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Nalo Shirikisho la
Vyama vya tiba asili nchini(SHIVYATIATA)
limesema linakusudia kwenda mahakamani kutaka tafsiri ya sheria ya tiba asili ya namba 23 ya mwaka 2002 ambayo imetoa mwongozo
wa tiba hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
Salaam,Mwenyekiti wa (SHIVYATIA)Abdulrahaman Lutenga amesema hawakubaliani na
hatua ya Dr Edmund Kayombo ambaye ni mwenyekiti
ni Baraza la Tiba asili, jambo linalowasukuma
kwenda mahakamani ila mahakama itoe tafsiri ya sheria ili haki itendeke kwani hatua ya kufungiwa kwa taasisi hizo kumejaa siasa,
Lutenga
amesema hatua Dr Kayombo ya kuvifuta usajili
vituo vya tiba asili huku vengine
kufungiwa kwa miezi sita hatua hiyo
imekiuka sheria 23 ya mwaka 2002 ambayo inataka hatua ifuatwe.
Amefafanua vifungu hivyo kuwa kuwa Uamuzi unaweza kutolewa na Baraza na bila ya kuwa na kikao cha kuwapelekea wajumbe nakala za shauri linalotakiwa kutolewa uamuzi wa kutoa maoni yao kwa maandishi,
Lakini pia amesema mjumbe yeyote anaweza kutaka uamuzi uhahirishwe na suala hilo lijadiliwe katika kikao cha baraza lakini changushangaza kifungu hiko mwenyekiti huyo hakuzifuhata.
Amesema sanjari na hiyo pia hata maamuzi hayo
hayakuzingatia taratibu na sheria namba 23
ya tiba asili na mbadala ya mwaka 2002 sura ya nne kifungu cha 23 ukrasa wa 28.
"Amekiuka sheria ,na hata ukiangalia maamuzi yake
hayakuzingatia misingi na miiko ya tiba asili iliyojikita katika mila,desturi na
utamaduni wa kitanzania yenye makabila zaidi 123”amesema Lutenga.
Amesema hatua
ya Baraza hilo kuvifungia vituo hivyo vitaleta athari kubwa kwa jamii kwani
vilikuwa vimetoa ajira ya watanzania zaidi ya 3000 huku pia zikiwaponya
watanzania masikini wanaotumia tiba hizo.
“Leo vituo vilivyokuwa na wafanyakazi zaidi ya 3000
leo unavifungia tena kwa kurupuka unategemea hawa watu wataishi vipi,harafu
tena ukiangalia watanzania wanaotumia tiba za asili ni zaidi alimia 80 ya watanzania, leo
unafungia vituo hawa watanzania masikini na wanyonge watapa tiba
wapi,tunamuomba Rais Magufuli alitazame hili”amesema Lutenge.
Hata hivyo,Lutenga amesema licha ya baraza hilo
kuchukua hatua hiyo amezidi ziomba Mamlaka husika kuwaondoa wafanyakazi kwenye
baraza hilo kwani hawana dhamira ya kuendeleza tiba asili na tiba mbadala.
Aidha,Baraza hilo limemwomba Waziri wa Ummya Mwalimu kuwangalia kwa makini watendaji baraza hilo kwani wamekuwa wakigongana.