SUMAYE AMUONYA TENA JPM,ASHTUSHWA NA MAISHA YA HOFU KWA WATANZANIA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye (katikati) akiwa anafurahia fomu ya kuwania uenyekiti wa Mkoa wa Pwani, aliyokabidhiwa na Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (kushoto) na Mwanasheria wa waziri huyo, Aidan Kitare |
FEDERICK Sumaye, Waziri Mkuu mstaafu amesema
anatamani kuona ndoto yake inatimia kwa Watanzania kubadili uongozi bila hofu
na vitisho vinavyosababishwa na watawala kwa kutumia nguvu ya dola, anaandika
Mwandishi Maalum.
Sumaye ambaye pia ni Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Cha cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameyasema hayo kutoka
na historia za baadhi ya viongozi wa Bara la Afrika pindi wanapoingia
madarakani kutopenda hata kuwaona wengine wakiinua pua.
Akizungumza
na wandishi wa habari Kijijini kwake mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea
nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mwenyeketi wa Dar es Salam, ,
Kijijini kwake Tondoroni, Kiluvya Pwani, Sumaye, amesema kuwa ni wakati sasa wa
kukipeleka chama hicho hadi katika ngazi za vitongiji ambako ndiko wanakoringia
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema
ni vema watawala wa kiafrika wakawaacha wananchi kutumia demokrasia yao katika
kujiamulia kuchagua kiongozi wanayefikiria atatekeleza malengo yao
wanayoyatarajia.
“Ndoto
niliyo nayo ni ile ile iliyonitoa CCM, katika demokrasia kwa mfano ukienda
Marekani huwezi kuona wamarekani wamekiacha CHAMA kimoja kikitawala miaka 30
hadi 40 kwaza hata miaka nane ni bahati sana kwa sababu chama kikitawala miaka
nane huwa ni bahati kwasababu wanaju kikishatawala miaka hiyo kitakuwa kimepata
fursa ya kutekeleza malengo yake,”amesema Semaye.
Amesema
tatizo lilipo Tanzani ni chama kilichopo madarakani kutokubali kuviona vyama
vingine vinainua pua ifike pali kwa chama tawala kukubali kushindwa pindi
wananchi wanapoamua.
“Kwa
kawaida chama chochote kikitawala muda mrefu hakiwezi kufanya vizuri na hiyo ni
sawa na anayepiga maji wakati hajui kuogelea hali inayowanyima wananchi fursa
ya maendeleo,”alisema Sumaye.
Sumaye,
amesema ndoto yake nikuona Chadema ina wafikisha Watanzania kule
wanakotaka na kuamini kwamba sasa demokrasia imechukua mkondo wke.
Akizungumzia
uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Sumaye, amesema anawashukuru
wanachama hao kwa kuonesha imani kwake na kuahidi kwamba yuko tayari kufanya
kazi ya kukiimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya chini kabisa.
Amesema,
ingawa ili awe mwenyekiti ni lazima achaguliwe lakini aliwaahidi wanachama hao
kwamba Chadema inahitaji kuongoza dola kwa hiyo kazu kubwa iliyoko ni wanachama
wa chama hicho kujipanga kuanzia sasa ikiwemo kujiepusha na migogoro isiyokuwa
ya lazima.
Amesema
haata inapotokea ni vema zikatumika busara katika kuipatia ufumbuzi ambayo
matokeo yake ni kuwa na chama imara.
“Nawashukuru
kwa kunichangia sh. 100000 ya kunichukulua fomu najuamefanya hivi kwa upendo
wenu wala siyo kwa ubaya nami nasema nimekubali ombi lenu Bali naomba mnipigie
kura msiishie hapa,”amesema Sumaye.
Naye
mwanasheria wake Aidan Kitare amesema kwa vile kesho ndiyo siku ya mwisho
atajitahidi pamoja na mgombea wake wanakamilisha utaratibu na kurusisha fomu
hiyo kabla ya saa 6:00 mchana.
Mwita
waitara mwenyekiti wa Dar es Salaam Kuu aliyekuwepo katika kumsindikiza
kiongozi huyo, amesema wanachama hao waliyojitokeza kumchukulia fomu Sumaye
walifanya hivyo wakiamini kwamba atakisaidia chama kwa vile anauzoefu mkubwa
katika masuala ya uongozi katika utumishi wa Umma.