Ajira Mpya 71,496 zasitishwa kisa watumishi HEWA
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Angella Kairuki amesema serikali imelazimika kusitisha ajira mpya
za watumishi 71,496 serikalini, mwaka huu hadi pale tatizo la watumishi
hewa litakapopatiwa ufumbuzi.
Akifungua
mafunzo kuhusu maadili ya viongozi wa umma kwa wakurugenzi watendaji wa
halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji Ikulu Dar es Salaam
jana, Kairuki alisema tangu oparesheni ya kutafuta watumishi hewa ianze
hadi sasa watumishi 12,246 wameshaondolewa.
Kairuki
alisema tatizo la watumishi hewa nchini bado ni kubwa kwani uzoefu
unaonesha kuwa nchi nyingi zilizokumbwa na tatizo hilo, ni asilimia
ndogo tu ya watendaji ndio iliyokuwa inawajibika.
Alisema
kwa sasa serikali imelazimika kusimamisha masuala mengi ya utumishi wa
umma ili ipate taarifa kamili ya aina ya watumishi waliopo, na kwamba
ma-DED hao kuhakikisha wanasimamia vyema oparesheni hiyo kwani hadi sasa
watumishi hewa waliobainika, takribani asilimia 90 wanatokea katika
Serikali za Mitaa.
Aidha,
Kairuki alisema pamoja na kugundulika kuwa tatizo la watumishi hewa ni
kubwa nchini, pia serikali imebaini kuwepo kwa watumishi watoro
wasiotimiza wajibu wao.
“Nawataka
mkahakikishe mnawabana hawa maofisa utumishi, haiwezekani kuwepo na
tatizo la watumishi hewa kubwa kiasi hiki huku pia kukiwa na tatizo la
watumishi watoro, hawa maofisa kwani walikuwa na majukumu gani?” Alihoji Kairuki.
Alisema
endapo serikali itabaini kuwa maofisa utumishi hao wamehusika katika
matatizo hayo ya watumishi hewa na utoro, wataondolewa mara moja.
“Serikali haina mchezo kila ofisa katika eneo lake, awe ofisa elimu, afya na kilimo wafanye kazi zao,” alisema.
“Serikali haina mchezo kila ofisa katika eneo lake, awe ofisa elimu, afya na kilimo wafanye kazi zao,” alisema.